Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kubishana na wakubwa kuna gharama zake.
Ndugulile alitakiwa kujua kuwa yeye ni mwanasiasa, taaluma yake awaachie wataalam waliopo Wizarani
Hata kwa Trump huko tunaona. Ukitofautiana naye kidogo tu unatupwa nje. Siasa vs sayansi japo kujifukiza kumekuwepo tangu zamani na tumejifukiza tangia tukiwa watoto....
View attachment 1452221
 
Real Madrid bado wana nia ya kumnunua Erling Braut Haaland na watamfuatilia mshambuliaji huyo wa miaka 19- leo Jumamosi wakati Borussia Dortmund watarejea uwanjani katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga. (Mundo Deportivo - in Spanish)
 
Lakini City wanataka kumuuza kiungo mshambulizi wa kati Leroy Sane msimu huu, licha ya masharti yao makali dhidi ya Bayern Munich kuhusu uhamisho wa Mjerumani huyo wa miaka 24. Mkataba wa Sane unaingia miezi 12 ya mwisho mwisho wa msimu. (Evening Standard)
 
Kiungo wa kati wa Ujerumani Toni Kroos, 30, amepuuzilia amble uwezekano wake kuungana tena na Pep Guardiola Manchester City ana amesema kuwa anatarajia kukamilisha taaluma yake ya soka katika klabu ya Real Madrid. (Eurosport)
 
Sergej Milinkovic -Savic anayenyatiwa na Tottenham Hotspur hana mpango wa kuitikia uhamisho wa lazima kutoka Lazio msimu huu. Mchezaji huyo nyota wa Serbia wa miaka 25 huenda akazawadiwa mkataba mpya wa mwaka mmoja wenye thamani ya £3.5m kwa uaminifu wake kwa klabu hiyo. (Corriere dello Sport via HITC)
 
Liverpool wako tayari kumnunua mshambuliaji wa miaka 17- Mbrazil Talles Magno. Kinda huyo ambaye usakataji kabumbu wake umelinganishwa Neymar, tayari anacheza katika kikosi cha kwanza cha klabu ya Brazil Vasco da Gama. (Mirror)
 
Newcastle wanafanya mazungunzo kuhusu uhamisho wa thamani ya £21.25m ya nyota wa Inter Milan Valentino Lazaro baada ya winga huyo wa Austria kuonesha umahiri wake alipokuwa wakicheza kwa mkopo katika klabu hiyo msimu huu. (Sun
 
Mkufunzi wa zamani wa Gunners Unai Emery anadai kuwa alilazimishwa kumsajili winga Nicolas Pepe, 25, kujiunga na Arsenal - na kufichua kuwa alimtaka mshambuliaji Wilfried Zaha, 27, baada ya kufanya mazungumzo na nyota huyo wa Crystal Palace. (Mail)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…