Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
10 Aorta (damu inatoka kwenda mwilini)
Siyo wafuasi tu. Ni cult kabisa (sijui neno cult kwa Kiswahili). Hawa hata afanye nini wao watamuunga mkono na kufuata kila anachosema. Wengi wao ni wazungu na wanaamini kuwa amekuja katika wakati muafaka kabla hawajazidiwa kwa uwingi na weusi pamoja na wahamiaji wengine. Ndiyo maana sera kuu iliyowavutia kwa huyu jamaa ni msimamo wake mkali dhidi ya wahamiaji pamoja na ahadi yake ya kujenga ukuta ili kudhibiti wahamiaji kutoka Meksiko na nchi zingine za Latin America. Wanadai wakizubaa tu America itakuwa kama Ulaya ambako utamaduni wa Kizungu umeharibiwa na wahamiaji hasa kutoka nchi za Kiislamu. Eti Ulaya sasa kuna misikiti mingi kuliko hata makanisa na hawataki hili litokee Amerika pia.
Kuna mvuvumko mkubwa sana kwa wazungu kusimama imara kujilinda kwa namna yo yote ile na kwao Trump ni shujaa aliyeletwa na Mungu ili kuwaokoa. Ndiyo maana sasa ubaguzi ni wa wazi wazi tu na kuna uhasama mkubwa kati ya weupe na watu wengine ambao siyo wazungu. Hawa ndiyo wadau wakubwa wa kauli mbiu ya Make America Great Again na hawataki Amerika kuhangaika na mambo ya nje huko. Ndiyo maana unaona Amerika ikijitoa katika mikataba mingi ya kimataifa na kusitisha michango yake ya kifedha katika mashirika mengi ya kimataifa. Nadhani huu ndiyo mwanzo wa mwisho wa America kama Global superpower kwa sababu huwezi kuwa superpower kama huna ushawishi wa kidiplomasia. Na Kirusi hiki Wachina wamecheza pele sana na wana nafasi nzuri ya kuziba mianya inayoachwa na Marekani kimataifa na hata kuibuka superpower wakitaka. Dunia ya wababe !!!
Cult kwa tafsiri yangu ni misukule