myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
Habari mbaya jirani. Namsoma Stephen Hawking hapa. Nimefika sura ya 9 katika kitabu chake mashuhuri cha Brief History of Time. Anasema kuwa haiwezekani kupunguza spidi ya wakati bila kuongeza spidi yetu. Na mfumo wetu tulionao katika universe hii mshale wa wakati daima unasonga mbele ndiyo maana tunakumbuka mambo yaliyopita na siyo yajayo. Kinadharia, hata hivyo, inawezekana kuwa na mfumo ambao mshale wa wakati unarudi nyuma. Katika mfumo huo tutakumbuka mambo yajayo tu. Hata hivyo mfumo huu utahitaji dhana mpya ya muda - imaginary time (muda dhahnia) na siyo huu muda tuliouzoea. Lakini pia pengine muda huu tulionao ni dhahnia pia kwa maana kuwa ni dhana tu tuliyonayo katika universe yetu hii...Siku Kuu imeshika kasi..