Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Utawala wa kidikteta huzaa tabaka la watu wachache wenye uwezo na kujenga ihramu ya kijamii ambayo madaraka, mali na fursa hujikita kileleni … kwa jina zuri zaidi, Ihramu ya Dhulma. Watawala wa kidikteta kwa msaada wa wafadhili wao wa kigeni hujenga dola tegemezi … Hii inasababisha mgawanyiko muhimu kwa wananchi … kwasababu zilizowazi na zilizofichika. (Qazi, 2011)
Lilikuwa jambo la kuchekesha namna tulivyolibaini jambo hili …Tulipowasili kutoka Moscow tuliwekwa hoteli Dar es Salaam. Siku ya pili yake tulikuwa tumeshughulika makao makuu ya jeshi. Hatukuwa na muda wa kuwasiliana na Babu au makomred wengine. Lakini kwa mshangao, kiasi cha saa 2 za usiku tulipoteremka chini kwenye ukumbi wa hoteli, nje ya varanda tuliwaona Babu, Badawi na Saleh Saadalla … Badawi ndiye aliyetoa siri kuwa tulikuwa hatutakiwi Zanzibar.
Lilikuwa ni jambo lililoandaliwa. Ijapokuwa ilikuwa ni jambo la kawaida kwa maafisa wa kijeshi kupangwa katika vikosi mbalimbali baada ya kumaliza mafunzo yao, kwetu sisi, madhumuni makubwa yalikuwa ni kupeleleza na kufuatilia mienendo yetu pamoja na kuzuia mawasiliano kati yetu na wenzetu wengine ambao walikuwa wanachama wa Chama cha Umma Party. Maafisa makachero wa kijeshi walipewa kazi ya kutupeleleza. Walitoa taarifa kuhusu mienendo yetu hapo makao makuu na makao makuu nao walitoa taarifa Zanzibar. (Mahojiano na Hamed Hilal, 2011)