Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama wengi wa wafuasi wa Karume waliokuwa waumini wa siasa za mrengo wa kulia, walikuwa ni watu waliotaka kulipiza kisasi na waliotoa hukumu za kesi kwa ukatili. Waliamua juu ya taratibu za mahakama bila ya kupingwa na mtu yeyote kwa kuwa mawakili hawakuruhusiwa kuingia katika mahakama hizo.

Kama alivyokumbuka Khamis, “Watu wengi walikamatwa na kupotea. Walikuwa wanaweza kukutia ndani. Halafu watakwambia, unawaona wale watu wanaotembea kule nje? Wale ni watu wazuri. Wewe upo hapa kwasababu una hatia .” Mahakama za wananchi zilibaki kuwa ndiyo muhimili wa mfumo wa sheria mpaka katika miaka ya 1980 (Mahojiano na Khamis Ameir, 2009).
 
Khamis anakumbuka kuwa alikuwa ni yeye tu peke yake miongoni mwa waliokuwa wanachama wa Chama cha Umma Party ambaye alibaki katika Baraza la Mapinduzi.

 
Kwa watu wengi wa Zanzibar, jambo baya kabisa wakati wa utawala wa Karume lilikuwa ni upungufu mkubwa wa chakula uliosababishwa na sera zake. Uchumi ulikuwa haukubadilishwa au kufanywa kuwa wa kisasa. Ulibaki kutegemea zao la karafuu kwa ajili ya kusafirisha nchi za nje na kuwa katika hatari ya kupanda na kushuka kwa bei katika soko la dunia. Lakini lililokuwa baya zaidi ni kuwa mapato yaliyopatikana kutokana na mauzo ya karafuu yalifichwa ili watu wa Zanzibar waendelee kupata shida hata wakati ambapo bei ya karafuu ilikuwa juu. Pesa zilifichwa katika tawi la London la benki ya Mosko ya Norodny Bank, wakati huo huo uagizaji wa chakula ulipigwa marufuku.
 
Ilipofika mwaka 1972 madhila ya watu yalikuwa makubwa kiasi ambacho, kama anavyoandika Chase:

 
Mnamo mwezi Februari mwaka huo Karume alipeleka ujumbe mzito Dar es Salaam kudai kuwa Babu arudishwe pamoja na wengine waliokuwa wanachama wa Chama cha Umma Party ambao walikuwa bara. Madai haya yalitokana na kuwa utawala wa Karume Zanzibar kila ulivyozidi kuwa ni wa kidhalimu, Babu alijitokeza kuwa ni mpinzani mkubwa wa serikali ya ASP.

 
Kuuliwa kwa Karume na Baada ya Hapo
Ilikuwa katika mazingira haya ya njama za hali ya juu za serikali, hali ya ukandamizaji uliokithiri visiwani Zanzibar na hasira za wananchi zilizozidi kupanda, ndipo Karume alipouawa tarehe 7 April, 1972. Watu wawili waliomwua Karume wote walikuwa wanachama wa zamani wa Chama cha Umma, Luteni Humud Mohamed, ambaye risasi zake ndizo hasa zilizomwua Karume na Kepten Ahmada. Kila mmoja wao alikuwa na sababu zake binafsi za kumwua Karume. Baba yake Humud aliuliwa akiwa gerezani, na inatuhumuiwa kuwa ilikuwa ni kwa amri ya Karume, na Ahmada aliteswa na serikali ya Karume mateso yaliyomsababisha atoe tuhuma za uongo. Humud na Ahmada, na watu wengine wawili ambao inasemekana walihusika na mauaji hayo, waliuliwa na polisi kufuatia kifo cha Karume.
 
Wakati Wazanzibari wengi inawezekana kuwa walifurahia, angalau kwa siri, kifo cha Karume, kilipelekea kuwepo kwa hali ambayo vibaraka ambao Karume aliwaamini sana na waliokuwa na vurugu kubwa wakiongozwa na Seif Bakari ndio waliokuwa kundi pekee lililokuwa na madaraka visiwani.

Hatimaye Aboud Jumbe aliteuliwa kuwa rais mwengine wa Zanzibar. Alikuwa ndiye mtu mwafaka aliyeteuliwa kwanza kwasababu alikubalika kwa kundi la Bakari na pili kwasababu hakuchukiwa sana na wananchi ukimlinganisha na wengi wengine waliokuwemo katika serikali ya Karume. Alikuwa ni mmoja miongoni mwa wasomi wachache waliovumiliwa na Karume, alikuwa mwerevu wa kutojali hata uonevu na ukatili wa dhahiri. Sasa alitumia werevu wake katika kutafuta suluhisho na makubaliano na serikali. Haya yalimwezesha pia kuimarisha nafasi yake, kuidhibiti na hatimaye kujikita kikamilifu katika madaraka yake.
 
Kikundi cha Seif Bakari kilichukua madaraka mara tu baada ya Karume kuuwawa na watu 1,100 walikamatwa na kutiwa gerezani katika siku chache zilizofuata. Miongoni mwao walikuwemo wengi waliokuwa wanachama na washabiki wa Chama cha Umma Party na wanachama wa ASP – wale waliodhaniwa kuwa wapinzani wa serikali ya Karume na kwa hivyo kuchukuliwa kuwa ni wapinzani wa kisiasa wa kikundi hicho.
 
Yaliyotokea kuanzia hapo mpaka kuanza kwa ile iliyoitwa Kesi ya Uhaini yalikuwa katika vipindi vinne vilivyofuatana. Cha kwanza kilikuwa ni cha kuwakamata na kuwahoji wale waliokuwepo kizuizini Zanzibar na ‘kukiri’ kwao baada ya mateso makubwa na baadhi ya wakati kwa maumivu ya kifo.

Cha pili ni kile cha kubuniwa kwa mpango mkubwa uliotokana na ushahidi unaotokana na ‘kukiri’ kwao huko. Madhumuni ya ‘mpango’ huo ambao unadhaniwa kuwa uliongozwa na Babu na Chama cha Umma Party, yanadaiwa kuwa yalikuwa ni kumwua Karume na baadae kuchukua madaraka visiwani.

Cha tatu, ni pale watu walipokuwa wakilazimishwa kukiri na ‘mpango’ huo kubuniwa kilikuwa ni kukamatwa kwa Babu na baadhi ya waliokuwa wanachama wa Chama cha Umma bara. Cha mwisho kilikuwa ni kuhojiwa kwa watu hawa, kuhojiwa ambako kuliandamana na mateso ya wawili kati yao, Hashil Seif Hashil na Hamed Hilal (mahojiano na Hamed Hilal, 2011).
 
Khamis alikamatwa tarehe 18 April, 1972, akiwa kada wa mwisho wa Chama cha Umma kukamatwa Zanzibar baada ya mauaji. Alikuwa ni yeye pekee aliyebakia katika Baraza la Mapinduzi na kama alivyonieleza ‘ ni rais tu ndiye aliyeweza kutia saini ili mjumbe wa Baraza la Mapinduzi akamatwe. Kwa hivyo, mara baada ya Jumbe kuwa rais, nilikamatwa na kutiwa gerezani ambako niliwakuta makomred wenzangu wengine huko!’ (mahojiano na Khamis Ameir, 2009).
 
Alipofika gerezani Khamis aliyakuta mateso yakimsubiri. Walifanyiwa vitendo vya utesaji wa kinyama hadi watu watatu – Musa Abdalla Ali, kwa umaarufu wake akijulikana kwa jina la ‘Meki’, Luteni Ali Othman na Abbas Mohamed, wote hao wakiwa ni watu waliokuwa wanachama wa Chama cha Umma Party – walikufa hata kabla ya kesi kuanza. Wengine, miongoni mwao wakiwemo Saleh Ali na Mohamed Saghir, walikufa mara baadae.
 
Chumba cha kuhojiwa, kwa mujibu wa maelezo ya mshitakiwa mmoja, ‘kilifanana na machinjio yaliyotapakaa damu ya binadamu’ (Chase 1976: 24). Mateso mengine yaliyofanyika yalikuwa ni pamoja na ukatili wa kijinsia, kulazimishwa kusimama huku mtu akiwa amefukiwa hadi shingoni katika mchanga au matope, ukatili wa kisaikolojia: kuwekwa katika chumba cha mahabusu nyoka waliotolewa meno, mahabusu kuvyetuliwa risasi kutoka kila upande, kuning’inizwa kwenye kamba iliyozungushwa shingoni na kutegewa kwa namna ambayo isingeliweza kuua (mahojiano na Khamis Ameir, 2009).
 
Mara kadha mwaka 1972, ‘Dourado [mwanasheria Mkuu Wolfgang Dourado aliyekuwa mwendesha mashtaka ] akija katika chumba cha kuhojiwa’, Khamis aliniambia, ‘husoma maelezo yaliyoandikwa na baadae kusema, “Inabidi mumkamue zaidi mtu huyu”, yaani mateso zaidi. Mahakamani alisema, “mikono yao ilisokotwa tu, basi,” kusema kweli, maelezo ya Dourado juu ya mada hii yanastahili kunukuliwa yote kwa ukamilifu. Yanaonyesha mtazamo wa matukio yanayofanana na hayo ya hivi sasa katika kesi za wale walioshtakiwa kwa mujibu wa sheria za ugaidi za Uingereza na Marekani. Hapa pia, matumizi ya ushahidi uliopatikana kwa njia ya mateso ni jambo la kawaida.
 
Wakati wa kesi, wale waliokubali makosa katika maelezo yao waliyakataa makosa hayo. Walieleza kuwa maelezo hayo yalipatikana kwa namna isiyo sahihi na kwa hivyo hayakuwa maelezo yaliyotolewa kwa hiari. Kwasababu, ya namna ya hali ilivyokuwa wakati wakutoa maelezo hayo walilazimishwa kukiri makosa na kutunga uongo na wakati mwengine maafisa wa upelelezi waliyaongezea maelezo yao ili kuipa kesi uzito mkubwa zaidi dhidi yao. Swali linalojitokeza kwanza ni kuwa, maelezo haya yanakubalika kisheria? Jibu fupi kwa swali hili ni kwamba kwa kuwa hayatakubalika chini ya mifumo mingine ya sheria, mfumo wetu hauna kizuizi cha kuzuia kukubalika kwa maelezo kama hayo. Mheshimiwa ataona kuwa ninakiri kwamba umekuwapo usokotaji wa mkono kidogo (utumiaji wa nguvu) ili maelezo haya yapatikane. (Chase, 1976: 24)
 
Kamatakamata, Kuweka Gerezani na Mateso Bara
Baada ya takriban mwaka mmoja wa mahojiano ya kikatili yaliyoambatana na mateso kwa wale waliotiwa gerezani, serikali hatimaye iliyapata matilaba yake ya kuwafanya wahojiwa ‘wakiri’. Kabla ya hapo, siku sita tu baada ya mauaji, makada wote wa kile kilichokuwa Chama cha Umma Party ambao wakiishi bara, pamoja na Babu, walikamatwa na kuwekwa gerezani.

Wakati akikamatwa, Babu alikwishajua kuwa alikuwa hatarini, kwasababu wakati wa maziko ya Karume, tarehe 10 April, tayari zilikuwepo dalili za nini kingelitokea. Edington Kisasi, kamishna wa polisi, alimwambia Mohammed Sahnun, Mualgeria aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika aliyekuja kuhudhuria maziko hayo, ‘tutampata Babu, akiwa hai au amekufa’ (Babu: 1975; 1).
 
Sahnun alishtuka na alipowasili Dar es Salaam wakati akirudi Algeria, alimtumia ujumbe Babu akimweleza kuhusu tishio hilo ovu. Hapo hapo, Babu alimwarifu Makamu wa Rais, Rashid Kawawa na kumtaka achukue hatua zinazofaa. Alitaka vile vile kumwona Nyerere, lakini ombi lake, kama Babu alivyokumbuka, lilikataliwa kwa utovu wa adabu mkubwa (Babu, 1975: 2).

Kukamatwa ambako Babu alikwisha tahadharishwa nako kulikuwa kwa namna ya kikatili. Kama alivyoandika katika barua aliyoituma kwa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa:
 
Tarehe 13 April, saa tisa alfajiri, nyumba yangu ilizungukwa na polisi wa kijeshi. Wakiwa na silaha nyingi na kwa mtindo ule ule wa Kigestapo walisukuma mlango wa nyumba yangu kwa jina la sheria na utulivu, walinikamata na kunifunga pingu, na kuzielekeza kichwani kwangu bunduki zao za rashasha zilizokuwa na risasi ndani.
… Ijapokuwa sikuonyeshwa hati yoyote ya kukamatwa au hati ya kunisachi, au kuelezwa kikosi hiki cha kinyama kilikuwa ni kwa ajili ya nini, hata hivyo, kikundi cha makachero kiliingia ndani wakiwa pamoja na wanajeshi waliokuwa na silaha na kuanza kuvurugavuruga kila kitu ndani ya nyumba yangu na kuchukua kitu chochote ambacho walidhani wanakitaka …Wakati wakiendelea kuvuruga kila kitu ndani ya nyumba yangu waliniamuru nitoke nje … huku nikiiacha familia yangu iliyokuwa katika hofu. Sikuwa na chaguo lolote. Walikwishanifunga pingu kwa hivyo waliniburura na kunitoa nje ya nyumba, kwa mabavu na kunivurumisha ndani ya gari lililokuwa likisubiri, ndani yake wakiwemo wanajeshi zaidi waliokuwa na silaha. (Babu, 1975: 2)

 
Alipelekwa katika gereza la Ukonga ambako kwa muda wa wiki mbili aliwekwa peke yake kabla ya kuhamishiwa gereza la Tabora kupitia gereza la Dodoma huku akiwa amefungwa minyororo. Gerezani Tabora, Babu alitupwa katika ‘chumba cha wale waliohukumiwa kifo’ karibu na chumba cha kunyongea. Alikaa hapo kwa muda wa miezi kumi ambayo saba katika hiyo akiwa ametengwa katika hali ya upweke. Katika kipindi chote hiki hakuambiwa sababu ya kuwekwa kwake kizuizini ijapokuwa kwa mujibu wa Sheria ya Kuweka Watu Kizuizini alikuwa na haki hiyo, kama zipo chache nyengine kwa vile sheria hii ya kikoloni (ambayo bado imo katika vitabu vya sheria vya Tanzania ) inawanyima wale waliofungwa jela chini ya sheria hiyo takriban haki zote za kiraia.
 
Siku hiyo hiyo, makada wote waliokuwa bara wa kile kilichokuwa Chama cha Umma Party, walikamatwa vile vile. Hamed Hilal, aliyekuwepo Dar es Salaam, alikamatwa pamoja na mke wake Fatma. Walipelekwa gereza la Keko ambako maafisa wengine wa jeshi kutoka Zanzibar waliokuwa wakifanyakazi bara walikuwa tayari wamekwishawekwa ndani. Hamed alinambia:

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…