Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tanga ni mji wenye kubeba historia kubwa ya mwanzo wa Taifa hili la Tanzania. Tanga imetajwa katika baadhi ya kumbukumbu za mabaharia wa Kireno walioanzisha kituo cha kibiashara eneo hili kwenye karne ya 16. Kwenye karne ya 18 Sultani wa Oman aliweza kuwapiga Wareno na kuwaondoa na kushikilia ukanda wa bahari ya Afrika ya Mashariki.
 
Tanga ikaendelea kuwa kituo cha biashara ya pembe za ndovu na watumwa. Mnamo karne ya 18 Wajerumani walinunua ardhi yote ya ukanda wa bahari wa iliko Tanzania bara sasa na kuufanya mji wa Tanga kuwa kituo cha kampuni yao iliyoitwa German Ostafrika na baadae mwaka 1891 mji huu ulikuwa wilaya ya kwanza na makao makuu ya kwanza ya utawala wa Wajerumani kabla ya kuhamia Dar es Salaam.
 
Makao makuu ya jeshi la Wajerumani yalikuwa hapa, shule ya kwanza ya serikali ilianza hapa na iliitwa Tanga School. Mtaalamu wa mimea wa Kijerumani, Dr. Hindrof aliweza kusafirisha kwa siri miche ya katani, kutoka Yucatan Mexico, aliweza kuisafirisha kwa kuificha ndani ya tumbo la mamba aliyekufa. Miche 66 ilifika salama na hiyo ndiyoilionzisha kilimo cha mkonge nchini, kikianzia Tanga
 
Kilimo cha mkonge kiliufanya mji huu kukua na pia kuwa na mchanganyiko wa makabila mbalimbali kutoka kila kona ya Afrika Mashariki, kusini mwa Afrika na Afrika ya kati, na pia kulikuweko na watu wa mataifa mbalimbali kutoka Asia na Ulaya. Mchanganyiko huu wa watu wa makabila na mataifa mbalimbali uliufanya mji huu kuwa na shughuli nyingi mchanganyiko za burudani za asili na nyingine mpya zilizotokana na watu wa tamaduni tofauti kukutana
 
Tanga ulikuwa mji wa vijana na kuwa na starehe nyingi sana ambazo zilizaa vikundi vya muziki wa aina mbalimbali. Kama nilivyosema awali kulikuwa na mchanganyiko wa makabila na hivyo makabila mbalimbali yalitengeneza vyama vyao kimoja wapo kiliitwa Young Nyamwezi Club, maarufu kama Yanga Nyamwezi na hawa ndio kilikuwa chanzo cha bendi ya Jamhuri
 
Wakati wa kuzaliwa kwake iliitwa Young Nyamwezi band, pia kulikuweko na bendi nyingine zinazokumbukwa mpaka leo kama Atomic Jazz, Amboni Jazz Band, White star Jazz band na kadhalika, huwezi kuzungumzia historia ya muziki wa Tanga bila kutaja vikundi vya taarab vya Lucky Star na Black Star.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…