Muziki wake ukawa maarufu na kujulikana kama mwanamuziki wa midundo ya ‘Nashville’ (ambayo ni mchanganyiko wa muziki wa zamani wa country na ule wa kisasa).
Wasifu wa nguli huyo unaonesha kuwa jina lake halisi alikuwa ikiitwaJames Travis aka “Jim” Reeves aliyezaliwa Agosti 20, 1923 Reeves amezaliwa katika kitongoji cha Galloways huko Texas, nchini Marekani.
Reeve alikuwa akitoka katika jamii ya watu waliokuwa nje ya mji karibu na Carthage. Alifariki Julai 31, 1964 akiwa na umri mdogo wa miaka 40 katika ajali ya ndege binafsi.
Licha ya kuwa na weledi katika muziki Reeves pia alikuwa mwanariadha aliyewahi kuchezea ligi za Semi-Professional kabla hajaingia mkataba na St. Louis Cardinals, timu ya shamba. Mwaka 1944 alicheza kama right-handed Pitcher.
Aidha alicheza ligi ndogo kwa miaka mitatu kabla hajaumia na kupata maumivu katika misuli iliyohitimisha juhudi zake za kuendelea na michezo.Reeves alianzia kufanya kazi kama mtangazaji wa radio.
Jim aliweza kufanya mitindo ya mwanzoni za bendi ya Mullican, nyimbo zake kama ‘Each Beat of My Heart’ na ‘My Heart’s Like a Welcome Mat’ mnamo miaka ya 1940 mwishoni na mwanzoni 1950.
Nyimbo zake za kwanza za ‘Country’ zilizompa mafanikio zilikuwa ni pamoja na ‘I Love You’ alouimba akishirikiana na Ginny Wright, na ‘Mexican Joe’ ‘Bimbo’.