Kwenye Ligi Kuu England, Liverpool imetumia Pauni 107.58 milioni taslimu kwenye usajili ndani ya muda huo na kujikuta wakishika namba 14 huko kwa matumizi ya pesa kidogo.
Klopp alisajili mastaa wawili kwa mkwanja unaozidi Pauni 70 milioni kila mmoja, beki Virgil van Dijk na kipa Allison ndani ya muda huo, lakini waliweka rekodi ya kuingiza Pauni 145 milioni kwenye mauzo ya Philippe Coutinho kwenda Barcelona, hivyo jambo hilo linawafanya kuwa na matumizi ya pesa taslimu Pauni 107 milioni tu kwenye usajili.
Chama la Frank Lampard, Chelsea ipo nafasi moja juu ya Liverpool, ikiwa na matumizi ya pesa taslimu, Pauni 115.57 milioni, licha ya kufanya matumizi ya pesa ndefu kwa kipa, Kepa Arrizabalaga.
Man City ndio wanaoshika usukani kwenye ligi kwa matumizi ya pesa taslimu na timu hiyo inayomilikiwa na bilionea Sheikh Mansour imetumia Pauni 601.98 milioni, huku baadhi ya mastaa iliyowasajili kwa pesa nyingi ni Riyad Mahrez, zaidi ya Pauni 60 milioni.
Nafasi ya pili wapo, Manchester United, waliotumia Pauni 484.88 milioni, huku ikiwa na mastaa kibao iliyowanasa kwa pesa nyingi akiwamo kiungo Paul Pogba na beki wa kati Harry Maguire.
Arsenal wanashika namba tatu kwa kutumia Pauni 267.88 milioni, na kwenye kikosi chake kuna mastaa iliyowanasa kwa pesa nyingi kama Nicolas Pepe na Pierre-Emerick Aubameyang.
Wakati wengine wa Big Six, Tottenham Hotspurl ambao hawajabeba taji lolote tangu waliponyakua Kombe la Ligi mwaka 2008, wao wametua Pauni 106.62 milioni, huku kwenye timu yao kukiwa na mastaa kibao iliyowanasa kwa pesa nyingi akiwamo Tanguy Ndombele na Mbrazili, Lucas Moura.
KANDA BONGO MAN ALIVYOTESA AFRIKA MASHARIKI.KANDA BONGOMAN NI MWANAMUZIKI AMBAYE KAMWE HATASAHAULIKA NA WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI HUSUSANI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM NCHINI TANZANIA.
WASIFU WA BONGOMAN UNAELEZA KUWA ALIZALIWA MWAKA WA 1955 KATIKA KIJIJI CHA INONGO, KILICHOPO NJE KIDOGO YA MJI WA KINSHASA HUKO JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO.