Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

mkutano mmoja kama huo (ulizungumzia katika ubalozi wa Marekani, 2009f chini ya kichwa cha habari ‘Zanzibar: wafadhili wataka kuwepo msimamo mmoja juu ya uchaguzi, mwafaka wa kisiasa’), ulihudhuriwa na mabalozi na mabalozi wadogo kutoka Uingereza, Norway, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Canada, Japan, Ubeligiji, Ireland, Italy, Hispania, Uswisi na Tume ya Ulaya, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini, wawakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na DFID ya Uingereza; mabalozi wadogo wa kisiasa kutoka Denmark, Norway, Sweden, Uingereza na Canada; na afisa wa ubalozi wa Marekani anayeshughulikia mambo ya Zanzibar.
 
(Inatubidi tushangae kwa nini Zanzibar ni muhimu kwa wawakilishi wote hawa wa nchi za magharibi.) Katika tukio hili, kama alivyoripoti balozi mdogo wa Marekani Mushingi:

 
Wiki chache baadae lilitokea jambo kuhusiana na uandikishwaji wa wapiga kura huko Pemba ambalo liliitia wasiwasi Norway. Simu za WikiLeaks zinafichua namna gani tukio hili liliwapelekea wanadiplomasia wajaribu ‘kucheza mchezo mchafu’ na CCM Zanzibar, mchezo ambao matokeo yake hayakuwa mazuri katika nyanja za kidiplomasia. Siku hiyo, wafuasi kadha wa Chama cha CUF wakielekea nyumbani baada ya mgomo wa amani uliofanikiwa dhidi ya uandikishwaji wa wapiga kura, uliotayarishwa na chama chao, walishambuliwa na Kikosi Maalumu cha Polisi, waliopiga risasi hewani kabla ya kuwafurusha na kuwakamata watu wawili na kumpiga mwengine mmoja vibaya sana.
 
Wakifadhaika kuwa hili lingeliweza kusababisha machafuko ya vijana, kuvurugika kwa uchaguzi na kumalizika kwa mategemeo yao ya kuwepo Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ‘Marafiki wa kundi la wanadiplomasia na wafadhili la 2010’ walitoa tamko, ambalo likitaka kufuatwa kwa viwango vya kimataifa na mchakato wa kidemokrasia katika mchakato wote wa uchaguzi wa 2010, likitilia mkazo hasa Zanzibar. Hata hivyo, kama ubalozi wa Marekani ulivyoiarifu Washington, Karume alijibu kwa dharau:

 
Marafiki walirudi nyuma. Kama ubalozi wa Marekani ulivyoieleza Washington, waliamua kuendelea kuichagiza Serikali ya Muungano na Rais Kikwete kudumisha amani na utulivu Zanzibar, na CUF kuepuka kuchukua hatua zisizo za kidemokrasia na vurugu. Na kukubaliana pia kuwa wafanye shughuli zao kwa hadhari ili kuepuka kuonekana kuwa wanafanya mambo yao kwa niaba ya CUF (na hasa kuepuka kuifanya CUF kuona hivyo), kwa kuwa ‘utegemezi wa CUF juu ya maoni ya kimataifa kunaweza kuwa ndiyo tishio la kulaaniwa vitendo vyao wenyewe na hilo kuwa ni nguvu kubwa kwetu’ (Ubalozi wa Marekani, 2009h)).
 
Zanzibar na Mustakbal Wake
Kikwete yuko tayari kuihakikishia tena Marekani kuwa yupo moja kwa moja chini ya miguu yao, na kuwa Tanzania, (Bara na Zanzibar) chini ya uongozi wake itayaweka mbele maslahi ya Marekani juu ya maslahi mengine yoyote. Hata hivyo, huko Visiwani mambo kidogo hayaeleweki kuhusiana na hilo, kwasababu ya kuzidi kuwepo hali iliyo dhahiri ya kutoridhika na uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na Bara.
 
Mwezi Septemba 2009, niliweza kufanya mahojiano na Juma Duni, wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF na ambaye mwenzake Ismail Jussa alimwelezea kwa wanadiplomasia wa Marekani kuwa ‘asiyetaka usuluhishi’ na ‘mwenye siasa kali’. Duni, mwenye ustadi wa kujieleza kwa ufasaha mkubwa (ambaye sasa ni waziri wa afya katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa na asiyezungumza sana kuhusu Muungano) aliainisha kutawaliwa na Bara kuwa ndiyo moja ya mambo ambayo yanakipa wasiwasi mkubwa chama chake.

 
Duni alikuwa na wasiwasi vilevile na masuala ya fedha:

 
Wakati huo huo, CUF na baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakisinikiza kuwa gesi na mafuta viwe chini ya udhibiti wa Zanzibar, na mwezi Oktoba 2012, hatimaye yalifikiwa makubaliano ya muda, yumkini vile vile chini ya shinikizo la makampuni ya mafuta na gesi. Mwezi Oktoba 2012 Zanzibar ilianza mchakato wa kuandaa mipango ya kisheria na kiasasi ya kusimamia mafuta na gesi yake (Bariyo, 2012)

Ikiwa mkataba utaridhiwa na yatapatikana mafuta yatakayokuwa na tija kiuchumi, hili litauathiri vipi mustakabali wa Zanzibar? Je, serikali itaweza kuuepuka mtego ambao umekuwa ni wa kawaida katika mikataba na kampuni za mafuta, kama vile kukataa kwao kulipa chochote isipokuwa sehemu kiduchu ya faida na posho ndogo kwa hasara itakayopatikana pindi ikitokea ajali? Ajali kama hizo zimekuwa ni jambo la kawaida katika Afrika, ajali ambazo husababisha hasara kubwa za kimazingira na kuwang’oa watu katika makazi yao ya kawaida.
 
Kwa mfano Tullow Oil ambayo tayari inafanya shughuli zake Tanzania, ilikuwa na uvujaji mkubwa wa mafuta nchini Ghana mwaka 2009 na 2010 (Platform, 2012); Chevron Texaco ilimwaga mafuta kutoka katika kisima chake kilichopo baharini kaskazini magharibi ya Angola mwezi Juni 2002 na kuchafua mazingira ya fukwe na kuwafanya wavuvi kushindwa kufanyakazi (Habari za BBC, 2002);

na Statoil ambayo inatarajiwa kuwa mshiriki mkubwa Bara na Zanzibar hivi karibuni ilimwaga kiasi kikubwa cha mafuta katika mbuga za Urusi (Staalesen, 2012), Shell, ambayo hivi sasa inatafuta mafuta katika bahari inayoizunguka Zanzibar, ni ahasi katika umwagaji wake wa mafuta na yenye kujulikana kwa uchafuzi wa mazingira ya ardhi ya watu wa Ogoni katika bonde la Niger
 
Ushahidi uliofichuliwa mwaka 2010 pia umeituhumu Shell na kuhusika kwake katika upatikanaji wa fedha na vifaa kwa jeshi la Nigeria na Luteni Kanali Okuntimo [Mnaigeria] ambaye aliwaua wazee wanne wa Ogoni, tukio lililosababisha kuuliwa kwa kiongozi wa watu wa Ogoni Ken Sero-Wiwa (Rowell na Lubbers, 2010).

Kuna swali vile vile la je! Ni nani hasa atakayenufaika nchini Zanzibar. Takriban katika kila nchi yenye utajiri wa mafuta katika Afrika limejitokeza miongoni mwa wanasiasa tabaka la walanguzi mafisadi wenye utajiri mkubwa na ambao wamekuwa wakishirikiana na mashirika makubwa kuzima na kunyamazisha upinzani. Hadi sasa, juu ya kutokuwepo hali ya usawa kwa kiwango cha hali ya juu katika nchi, suala la kurekebisha hali kwa mgawanyo sawa wa rasilmali miongoni mwa watu wa Zanzibar halionekani kuwemo katika ajenda ya CUF wala ya CCM.
 
Huku viongozi wa CUF na CCM wakiwa katika malumbano makali baina yao wenyewe kwa wenyewe ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, madai ya kutaka Zanzibar iwe dola huru yametolewa kwa nguvu kubwa na chama kilichoandikishwa kuwa ni Asasi Isiyokuwa ya Kiserikali, Umoja wa Mpango wa Kuwaandaa Waisilamu, ‘Uamsho’.

Umoja huu uliwavutia Wamarekani tokea mwaka 2005 (Ubalozi wa Marekani, 2005a), huku Michael Owen, naibu wa ubalozi wa Marekani na balozi mdogo Dar es Salaam, akiuelezea umoja huo kuwa ‘wenye kelele zaidi miongoni mwa vyama vidogo vya wenye siasa kali Zanzibar … kinachojumuisha mashehe vijana wachache wenye mtazamo wa Kiwahabi wa Saudia …
 
Chama cha CCM kinauona Uamsho kuwa ni kivuli cha chama cha upinzani cha CUF. Owen aliendelea kuelezea ni vipi:

 
Ilipofika 2012 Uamsho haikuwa asasi ndogo tena. Mikutano yake ya hadhara iliwavutia maelfu ya watu na ilikuwa ikichukua msimamo wa kisiasa kwa uwazi kabisa, ikifanya kampeni dhidi ya Muungano na kuulaumu kwa kuifilisi Zanzibar kiuchumi. Vijana wasiokuwa na ajira na wasioona mustakabali wowote mbele yao na wenye kukasirishwa na hali inayoonakana wazi wazi ya kukosekana usawa wanavutiwa na kundi hili kwa wingi. Serikali imejibu hayo kwa kuzidisha ukandamizaji.
 
Mwishoni mwa mwezi Mei 2012, kanisa kubwa lililokuwepo nje ya mji mkongwe lilivamiwa na kundi la watu wenye hasira na kuunguzwa vibaya. Mara moja lawama ilitupiwa kikundi hiki, juu ya viongozi wake kukanusha vikali kuhusika kwa namna yoyote.

Haikutimia hata miezi miwili baadae wakati ilipozama meli iliyokuwa ikisafiri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar ambayo ilisababisha vifo vya watu wanaokisiwa kuwa 145 na serikali kulaumiwa kwa kushindwa kwake kusimamia kanuni za usalama, lilitokea tukio jengine kubwa.

Waombolezaji ambao baadhi yao walikuwa wafuasi wa Uamsho walikusanyika nje ya msikiti ili kuwaombea dua marehemu na hapo walivamiwa na polisi, wakarushiwa mabomu ya kutoa machozi, kupigwa na kukamatwa (Reuters, 2012).
 
Mnamo wiki ya mwisho ya mwezi Oktoba 2012, Sheikh Farid Hadi, kiongozi wa kidini wa Uamsho alipotea kwa muda wa siku tatu. Hasira za wafuasi wake zilizagaa barabarani. Kilichofuatia hapo yalikuwa ni mabomu ya kutoa machozi, mapigano ya barabarani na watu zaidi ya mia moja walikamatwa.

Polisi walisema kuwa hawakujua lolote kuhusu mahali alipokuwepo, lakini Hadi alipotokea tena, alisema kuwa alifungwa kitambaa machoni, alipelekwa mahali asipopajua na kuhojiwa kuhusu mipango ya baadae ya Uamsho na kuhusu ziara zake za mara kwa mara huko Oman na nchi nyengine za Kiarabu (Zakaria, 2012).

Wakati huo huo, Uamsho tayari ilikuwa ikielezwa katika vyombo vya habari, bila ya ushahidi wowote, kuwa ina uhusiano na Somalia au hata na Boko Haram, kundi la Waisilamu linalohusika na vita vikubwa vya kidini nchini Nigeria (Jorgic, 2012).
 
Nini kilichosababisha kuwepo kwa dira hii kwa mustakbal wa Zanzibar? Kusema kweli, Zanzibar ina mambo machache yanayofanana na Brunei, ambayo ni nchi ya kihafidhina ya Kiislamu inayotawaliwa na mfalme, ambayo Wamalay wa nchi hiyo wanaishi kwa jasho la wafanyakazi wasiokuwa raia. Labda matumaini haya yanaonyesha ukosefu wa taarifa.

Labda kuna dhana pia, kwa mbali, kutoka kwa wale wafuasi wa zamani wa siasa za mrengo wa kulia na waumini wa itikadi ya Chama cha ZNP ambayo inawaona wanachama na wafuasi wa Chama cha ASP kuwa ni wa kutoka nje na si Wazanzibari. Kwa namna yoyote ile, kuwepo kwa nguvu za Uamsho hakuwezi kupingika na pia namna ya kuungwa mkono kwake, hasa katika jamii iliyogawanyika kati ya Waarabu na Waafrika na katika mgawanyiko wa kitabaka vilevile.
 
Wakati kitabu hiki kinakwenda kwa mchapaji, serikali imeishambulia tena asasi ya Uamsho. Sheikh Farid Hadi na viongozi wengine wa asasi hiyo wamekamatwa na wapo gerezani, ambako wamekuwa wakidhalilishwa na kunyimwa haki za msingi za kidini – kwa mfano, wakilazimishwa kunyoa ndevu na kunyimwa fursa ya kusali sala zao za fardhi.

Wakati huo huo imeundwa kamati mpya ya watu sita ili kuendeleza mjadala huu. Kwa namna yoyote ile, wajumbe wake wanaunga mkono kuendelezwa kwa kampeni ya kuwa na Zanzibar iliyo huru iliyounganishwa kwa mkataba na Tanganyika iliyo huru (Machira, 2012).
 
Miongoni mwa wajumbe wake wengi ni wale ambao Marekani inawakubali: Ismail Jussa, aliyeshiriki katika Mpango wa Marekani wa Wageni wa Kimataifa, Eddy Riyami, mfanya biashara mashuhuri; Hassan Nassor Moyo (CCM) ambaye mchango wake katika miaka ya 1960 na 1970 nimeueleza katika kurasa za nyuma na aliyekuwa waziri Yusuf Himid.
 
Ambaye hayumo katika kamati lakini yupo karibu sana na kamati hiyo ni Salim Rashid ambaye hapo awali alikuwa mwanachama wa Chama cha Umma lakini baadae alibadili sana mtazamo wake na kusaidia kutayarisha, miongoni mwa mambo mengine, mpango wa mabadiliko ya kuleta mfumo huria uliofuatwa na Zanzibar mwaka 1984. Maoni ya Rashid juu ya mustakbal wa Zanzibar yamo katika makala ambayo yamekuwa kama ndiyo ilani ya mfumo huria mambo leo kwa ajili ya kamati hii na wanasiasa wengine wanaoshinikiza kuwepo kwa Zanzibar iliyo huru (Rashid, 2011).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…