Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mchezo wa kwanza utakuwa kati ya klabu ya Newcastle United walio kwenye hali mbaya kwenye msimamo wakiwa wanashika nafasi ya 14 wakiwa na pointi 35, wakapo waliika Sheffield United wanaoshika nafasi ya sita walio na pointi 44 majira ya saa 8:00 mchana.
 
Newcastle wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na changamoto ya ubutu kwenye eneo lao la ushambuliaji kwani, katika mechi mbili za mwisho hawakufanikiwa kufunga hata bao moja. Timu hizi pia zimekutana mata tatu ambapo Newcastle alifanikiwa kushinda mara mbili na Sheffield akashinda mara moja.
 
Ikiwa Newcastle itashinda, itapaa nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi, ambayo kwa sasa ipo Everton iliyo na kibarua kizito mbele ya Liverpool leo, wakati Sheffield United wao wakipata ushindi watapaa hadi nafasi ya tano na kuwashusha Manchester United ambao ndio wanashikilia nafasi hiyo kwa sasa.
 
Katika mchezo huo uliopangwa kuanza saa 10:15 jioni, Aston Villa wataingia na kumbu kumbu mbaya ya kupoteza michezo minne kati ya mitano waliyocheza hivi karibuni kwenye EPL huku wakitoka sare moja, Lakini Chelsea nayo itaingia ikiwa na rekodi ya kutoka sare michezo miwili, kupoteza mmoja na kushinda mitatu
 
Ikiwa Villa itashinda mchezo huo, itakuwa imejitoa kwenye nafasi ya 19, ambayo ndio wanashikilia kwa sasa, wakiwa na pointi 29, na kupanda hadi nafasi ya 15, pia Chelsea wao wakipata ushindi watabakia kwenye nafasi yao hiyo hiyo licha ya kufikisha pointi 51,
 
Mchezo wa mwisho kabisa utakuwa kati ya watoto wa Carlo Ancelotti watakaovaana na Liverpool katika dimba la Goodison Park. Mechi baina ya timu hizo ni miongoni mwa michezo ya EPL ambayo huwa na mvuto na ushindani wa hali ya juu kutokana na utani wa jadi uliopo baina ya timu hizo.
 
Mpaka unaotenganisha viwanja vya timu hizi mbili ni bustani tu, na hii ni moja ya mechi zinazotajwa kuwa na upinzani wa hali ya juu. Everton imekuwa na rekodi mbovu ya kutowahi kupata ushindi mbele ya Liverpool kwenye mchezo wowote tangu Januari, 16, 2011.
 
Everton wanaoshika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 37, ikiwa watashinda mchezo huo watapanda hadi nafasi ya tisa na kuishusha Arsenal, lakini pia Liverpool ikipata ushindi itakuwa inahitaji mchezo mmoja pekee ili watawazwe kuwa mabingwa rasmi wa Epl, wataweza kweli?
 
Back
Top Bottom