Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

VITA YA UMEME.

Edison aliendelea kusambaza umeme wake lakini alipata changamto kubwa kwa makampuni yaliyokuwa yakisambaza umeme geu (Alternating Current.) na hapo ndopo kukaibuka vita ya umeme kati ya Edison aliyekuwa akisambaza umeme mnyoofu (DC) na makampuni ya kusambaza umeme geu (AC).
 
Edison alianzisha kampeni ya kupinga makampuni ya umeme geu kwa hoja yake kubwa kwamba umeme geu ni hatari kwasababu una madhara kwa watumiaji kwasababu unatumia volti kubwa sana hivyo aliamini umeme wake ndiyo chaguo sahihi kwa wananchi kwasababu haikutumia volti kubwa sana.
 
Lakini baadae Edison alikuja kushindwa vita hivyo baada ya umeme wake kushindwa kuusambaza zaidi ya maili moja kutoka kwenye kituo cha uzalishaji hivyo alishindwa kuwafikia watu wengi maeneo mbalimbali, kwasababu alikosa njia ya kuongeza ukubwa wa volti za umeme mnyoofu (DC)
Hii ilikuwa tofauti kwa makampuni ya umeme geu (AC) yaliweza kusambaza umeme maeneo mengi hata ya mbali sana kutoka kwenye kituo cha uzalishaji ni kwasababu ya matumizi ya transifoma kupunguza na kuongeza ukubwa wa volti za umeme.
 
Thomas Edison alifariki akiwa ni mzee wa umri wa miaka 84 alikuwa akisumbuliwa na kisukari.
Thomas Edson alizikwa nyuma ya nyumba yake ambapo baadae palifanywa kuwa makumbusho yake ambayo yanafahamika kama Thomas Edison National Historical Park.
 
Biologia inatuelezea kwamba kwenye tendo la ndoa mbegu zinazotoka kwenda kwa mwanamke ni milioni 300 na uanza kukimbia kwenda kukutana kwenye ovum,
Mbegu mbegu 500 ndo uweza kufika sehemu husika tu(kwenye ovum)mbegu nyingne huchoka nakufia njiani,kati ya mbegu 500 zinazofanikiwa kufika na kushinda na kutengeneza kiumbe ni moja tu,mbegu iyo ni wewe unaesoma ujumbe huu.

Kama usingeshinda mbio zile,nakuwashinda wenzio milioni 300 usingekuwepo dunian leo.
umewai kufikiri juu ya hili??biologia inatueleza kwamba ulikimbia nakuwashinda wenzako milioni 300,bila macho,bila miguu bila mikono,ulikimbia mbio bila elimu yako na ukashinda,ulikimbia bila cheti ukashinda,bila msaada wa mtu yeyote na ukashinda,je ni kitu gani hukufanya hufikiri kushindwa kwenye maisha hadi kukata tamaa??

Leo hii unamacho,unamiguu,mikono una neno la mungu kwann ushindwe??kwann ukate tamaa??muombe mungu,kuwa na maono kisha weka mipango thabit,utafanikiwa usikate tamaa ata siku moja kwani ulishawai kuwa mshindi kwenye mbio za watu milioni 300 kwann ushindwe Leo??

Changamoto ni sehemu ya maisha lakini kamwe zisikukatishe tamaa,kuwepo kwako duniani ni mpango kamili wa mungu,hukuja duniani bahath mbaya lipo kusudi la uwepo wako,hakikisha unalitambua kusudi hili na kulitimiza,haijalishi unapitia wakati gani kwa sasa amini kwamba ulizaliwa kushinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…