Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1592887286542.jpg
 
_MFAHAMU THOMAS EDSON, MGUNDUZI WA TAA YA UMEME._Anaitwa Thomas Alva Edison mfanyabiashara na mgunduzi maarufu nchini Marekani, alizaliwa Ohio, Marekani mnamo mwaka 1847 tarehe 11 ya mwezi wa pili na kufariki mwaka 1931 tarehe 18 ya mwezi wa kumi.
 
Aliweza kusoma na kuandika na elimu yake nyingi aliipata kwa kujisomea mwenyewe vitabu mbalimbali, vilevile alikuwa akifundishwa mambo mbalimbali na marafiki zake aliokuwa akikutana nao.Thomas Edison alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya masikio na kuwa na usikivu hafifu hali hiyo ambayo ilionekana kusababishwa na homa kali ambayo ilimpata akiwa mtoto na kuugua masikio mara kwa mara pasipo kupata tiba yoyote.
 
Lakini Thomas Edison alikuwa akilihusisha tatizo lake hilo na kipigo alichokipata kutoka kwa kondakta wa treni ambaye alimpiga sikioni wakati akisafiri kwenye treni na kwa bahati mbaya kemikali zake alizokuwa akisafiri nazo ziliwaka moto kwenye buti la treni na kushushwa kwenye treni pamoja na makemikali yake
 
Thomas Edison alikuwa ni mfanyabiashara na mbunifu ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sayansi na teknolojia ulimwenguni.Maisha yake ya biashara yalianzia kwenye uuzaji wa magazeti ndipo alipojigundua kuwa na kipaji cha mfanyabiashara na baadae kuamua kuchapisha gazeti lake mwenyewe. Na baadae kumpelekea kuanzisha makampuni 14 ya shughuli mbalimbali ikiwepo kampuni ya General Electric ambayo mpaka sasa bado ni kampuni kubwa ya kibiashara duniani.
 
Thomas Edison alifanikiwa kubuni vitu mbalimbali kwa kuweza kufanya kazi zake katika timu, aliweza kukusanya watu na kushirikiana nao katika shughuli zake na ndiyo mgunduzi wa kwanza kuweza kufanya gunduzi zake kwa kutumia timu yake tofauti na wagunduzi wengine ambao wanakomaa wenyewe kimyakimya.
 
Thomas Edson alikuwa akiuza pipi na magazeti kwenye treni na baadae alikuwa msimamizi wa mawasiliano katika kituao cha treni kazi hii aliipata baada ya kumuokoa mtoto wa mkuu wa kituo wa miaka mitatu.
 
Baba wa mtoto huyo alipendezwa na Thomas Edison na kuamua kumfundisha jinsi ya kuongoza mitambo ya mawasiliano na kumpa kazi katika kituo hicho.Elimu yake aliyoipata katika kusimamia mitambo ya mawasiliano ilimpelekea kugundua kifaa cha kurekodia sauti ili kupata mawimbi mazuri ya sauti kwenye simu.Na safari yake ya ugunduzi ilianzia hapo.
 
_UGUNDUZI WA TAA YA UMEME._

Mnamo mwaka 1878, Edison alianza kazi yake ya kuhakikisha anapata mwanga unaotokana na umeme ambao utakuwa bora zaidi kuliko mwanga wa gesi na mafuta ambao ulikuwa unatumika miaka hiyo
 
UGUNDUZI WA TAA YA UMEME.

Mnamo mwaka 1878, Edison alianza kazi yake ya kuhakikisha anapata mwanga unaotokana na umeme ambao utakuwa bora zaidi kuliko mwanga wa gesi na mafuta ambao ulikuwa unatumika miaka hiyo
 
Edison alifanya tafiti nyingi sana alijaribu vitu mbalimbali kwenye umeme ili apate mwanga. Tarehe 22 mwezi wa kumi mwaka 1879 Edison alifanikiwa kwa mara ya kwanza kupata mwanga kutoka kwenye waya wa kaboni lakini mwanga huo iliwaka kwa masaa 13 na nusu pekee na taa ikaungua.
 
Baadae aliboresha taa yake na kuwa na uwezo wa kuwaka kwa masaa 1,200 tofauti na ile ya mwanzo.
Baada ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutengeneza taa ya umeme Edison na timu yake mnamo tarehe 17 Disemba 1880 alibuni na kupata haki miliki ya miundombinu ya kusambaza umeme majumbani.
 
Baadae aliboresha taa yake na kuwa na uwezo wa kuwaka kwa masaa 1,200 tofauti na ile ya mwanzo.
Baada ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutengeneza taa ya umeme Edison na timu yake mnamo tarehe 17 Disemba 1880 alibuni na kupata haki miliki ya miundombinu ya kusambaza umeme majumbani.
 
Back
Top Bottom