Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1593088047006.jpg
 
Roma imeanza kukaliwa na watu kwa zaidi ya miaka elfu 2 iliyopita.... Ni mji wa 3 kwa umaarufu katika nchi za umoja wa ulaya na ndani ya mipaka ya Roma ndio unapata Vatican City ambayo ni makazi ya kiongozi mkuu wa kanisa katoliki (ukumbuke Vatican ni nchi inayojitegemea)
 
Wengine wanapenda kuiita Roma kama Mji mkuu wa nchi Mbili

Roma iliendea miaka mingi iliyopita tokea karne ya 3 walishakuwa na mtandao wa babrabara, chuo kikuu kilianzishwa mwaka 1303 na duka kubwa la kuuza bidhaa mbalimbali (shopping mall) zilianzishwa tokea mwaka 110
 
Kutokana na mashaka na wasiwasi wa kuona huenda hawa watoto mapacha watakuja kumpindua na kuchukua madaraka yake alituma miongoni mwa wasaidizi wake awaue Romulu na Remo ....lakini msaidizi huyo hakuwaua na badala yake aliwatia kwenye kikapu na kuwaacha kwenye mto Tevere
 
Baada ya kazi hiyo kubwa waliamua kwenda kuanzisha mji wao

Katika kuanzisha huko mji wakatofautiana kwenye jina la mji watauitaje?? Kila mtu alikuwa na wazo Lake baadae wakapigana wenyewe kwa wenyewe na Romulu alifanikiwa kumuua Remo

Na hapo ndipo aliamua kuupa jina lake mji huo mpya

Tokea wakati huo mji ukawaitwa Roma

Na hii ndio asili ya jina la mji wa Roma
 
JUA MAAJABU YA MIJI ZILIZO CHINI YA BAHARI.
1-Lion City – Qiandao Lake, China
Mji huo ulifurikishwa maji kwa makusudi mwaka 1959 ili kujenga ziwa na kituo cha umeme kinachotumia nguvu za maji. Lion City (uliochukua jina la Lion Mountains) ulikuwa kituo cha kisiasa na kiuchumi mashariki mwa China.
 
3-Dwarka – India
Uko chini ya maji (futi 70) ambazo ni mita 21 karibu na kisiwa kinachokaliwa na watu cha Bet Dwarka. Mji huo wa zamani wa Dwarka ni hazina ya kweli ya zamani unayopaswa kuitembelea. Unakisiwa kuwa ulijengwa kati ya miaka 9,000 na 12,000 iliyopita.
 
Back
Top Bottom