Hata hivyo vyama vya upinzani vikiongozwa na Chakwera vilipinga vikali matokeo hayo na kwenda mahakamani.
Maandamano makubwa pia yalishuhudiwa katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo dhidi ya matokeo hayo. Waandamanaji hao walishinikiza mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jane Ansah ajiuzulu.
Mahakama ya katiba ikathibitisha kuwa kulikuwa na udanganyifu wa wazi katika uchaguzi huo na kubatilisha matokeo hayo mwezi Februari 2020 na kuamuru uchaguzi mpya ufanyike ndani ya siku 150. Bi Ansah akajiuzulu mwezi Mei kupisha uchaguzi mpya.
Katika uchaguzi wa wa 2019, wagombea sita wa upinzani walikuwa wakipambana kumng'oa Mutharika. Katika kura ya marudio iliyopigwa wiki iliyopita jumla ya vyama tisa vilimuunga mkono Chakwera katika umoja wa wapinzani unaofahamika kama Tonse.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.