Nimeshangaa wapinzani wa hapa kwetu wanashangilia huo ushindi. Huo ushindi ilitakiwa CCM ndio washangilie maana wenzao wameshinda kwa kuaminiwa na wananchi.
MCP ni chama cha ukombozi, kilitolewa madarakani na upinzani, baada ya miaka kupita wananchi wakachoka ulaghai wa wapinzani wakaona bora warudi (hawakuuona Kanaani wakaona warudi Misri) kule kule kwa zamani tena kwa nguvu ya umma.
Wapinzani wa hapa kwetu walitakiwa wachukue kama somo kutoka kwa wenzao kwa kutokuaminiwa na walio waaminisha kuwa utawala wa Banda (Magu) na chama chake MCP (CCM) ulikuwa mbaya kwa kutokuwakomboa kutoka kwenye dimbwi la ufukara.
Ushindi wa MCP wana CCM wamenuna wakati walio shinda ni wakombozi wenzao ila kushindwa kwa DPP wana CDM wanashangilia wakati walio shindwa ni wanamageuzi wenzao [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]