Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukifika wakati wa KUACHANA sio lazima MGOMBANE. Kuna wakati itabidi uachane na mbia wako (Business Partner) wa biashara ambaye mlipanga kufika mbali sana. Kuna wakati itabidi uachane na bosi wako ambaye ndiye alikusaidia kukufundisha kazi hapo mwanzo. Kuna wakati itabidi uachane na mtu uliyekuwa unampenda sana na ulidhani utakuwa naye kwa muda mreeefu. Kuna wakati katika maisha utalazimika kuachana na watu, ofisi, chama cha siasa n.k. Ukifika wakati huu kuna mambo ya kuzingatia. Moja, sio lazima UANZISHE UGOMVI na unaoachana nao. Unaweza kuachana kwa HESHIMA na UTULIVU. Kumbuka kuachana sio VITA, mnaweza kuachana na maisha yakaendelea. Sio lazima uwageuze ADUI wale unaowaacha au wanaokuacha. Maisha yana majira na kila mtu anatakiwa kuwa mahali fulani kwenye majira tofauti. Mbili, pokea maumivu na yakubali. Haitasaidia kutokubali uhalisia. Kama mtu ameamua kuondoka, hakuna namna. Haitasaidia kukataa uhalisia, badala yake jipange kwa hatua inayofuata. Tatu, usijilazimishe kuonyesha ubaya wa unayeachana naye. Kumbuka mafanikio ya UNAKOKWENDA hayajabebwa na watu kujua ubaya wa UNAYEACHANA naye bali yamebebwa katika DHAMIRA SAFI ya UNACHOKWENDA KUFANYA. Hakuna umuhimu wa kumpaka matope unayeachana naye. KUACHA au KUACHA kunauma ila MAISHA LAZIMA YAENDELEE.
 
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Joseph Shila mwenye miaka 29 Mwalimu wa Shule ya Msingi Mwakaleli, Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe, kwa tuhuma za wizi wa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 34 za Mwalimu Mstaafu Gideon Mwalujobo mwenye miaka 60 Mkazi wa Mwakaleli‬
 
MWIGIZAJI WA GHANA ALIYEPIGA PICHA ZA UTUPU NA MTOTO WAKE; AOMBA RADHI. Mwigizaji wa Ghana wa Rosemond Brown maarufu kama @akuapem_poloo ameomba radhi baada ya kupost picha ya utupu (kama alivyozaliwa) akiwa na mtoto wake wa miaka saba. Akuapem Poloo alipost picha hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram Jumatatu, Juni 30, 2020 kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wake aliyetimiza miaka saba. Watu mbalimbali, vyombo vya habari, walimtuhumu mwigizaji huyo pamoja na mashirika kadhaa ya asasi za kiraia, na Shirika la Haki ya watoto ya Kimataifa kuitaka Idara ya Upelelezi wa Jinai ya Polisi (CID) ya Huduma ya Polisi ya Ghana kuangalia jambo hilo kuwa ni kama uvunjaji wa kanuni ya ustawi wa Sheria ya Mtoto. Pamoja na kuomba msamaha alisema; Yeye huoga bafuni pamoja na mtoto wake huyo kila wakati.
 
GWAJIMA Atangaza NIA KUGOMBEA UBUNGE Jimbo la HALIMA MDEE... ASKOFU wa kanisa la Ufufuo na uzima, Josephat Gwajima, leo Julai 01, ametangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kawe kupitia (CCM) Jimbo hilo kwa hivi sasa lipo chini ya Mbunge wa Chadema, Halima Mdee..
 
Bwana Trump aliulizwa pia kama anaamini bado kuwa virusi vya corona siku moja ''vitatoweka''.

''Ninaamini'' alisema .Ndio hakika, Wakati wa sherehe zijazo za uhuru tarehe 3 mwezi Julai, watu watakaohudhuria wanaomuunga mkono hawatalazimika kuvaa barakoa wala kulazimishwa kutochangamana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…