Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1594457643258.jpg
 
Mary anaandika kwamba Trump Sr alikuwa mkali sana kwa mtoto wake wa kiume mkubwa (yaani baba yake), ambaye alitaka achukue majukumu ya kusimamia biashara ya familia ya uuzaji wa nyumba. Lakini kadiri baba yake Mary alivyokuwa anaendelea kujitenga na maswala ya biashara ya familia, Trump Sr, hakuwa na la kufanya zaidi ya kukimbilia kwa kijana wake mdogo, Donald.
 
Halikuwa chaguo la kufurahisha, Bi. Trump anasema.

"Mambo yalipoanza kwenda mrama mwishoni mwa miaka 1980, Fred alishindwa kujitenganisha na ukatili na udhaifu wa kijana wake na akalazimika kuendelea kushikilia biashara," ameandika kuhusu tabia ya Trump Sr, kwa rais wa 45 wa Marekani.
 
"Jinamizi wake alikuwa huru."

Ikulu ya Marekani ilikanusha madai kwamba baba yake Trump alikuwa mkali, akisema kuwa rais anaelezea uhusiano aliokuwa nao na baba yake kama wa amani na kwamba baba yake alikuwa mzuri sana kwake".
 
Ni lazima nimfichue Trump'

Katika kitabu hicho, Bi. Mary anaelezea vile alivyowasilisha nyaraka za kodi kwa gazeti la New York Times, iliyozitumia kuchapisha makala ya uchunguzi ya maneno 14,000 kwa mifumo ya kodi ya miaka ya 1990 ya Trump ikiwemo ulaghai, ambao uliongeza utajiri aliopata kutoka kwa wazazi wake.
 
Alidanganya kuingia chuo kikuu'

Bi. Mary anadai kwamba mjomba wake alimlipa rafiki yake ili amfanyie mtihani kwa niaba yake - mtihani wa kitaifa ambao unaamua chuo kikuu mtu atakachokwenda kwasababu alikuwa na wasiwasi kwamba alama zake za wastani ambazo zingekatiza juhudi zake za kukubaliwa.
 
Back
Top Bottom