Vyakula bora ni dawa tosha kwa miili yetu. Ulaji wa vyakula vyenye virutubisho vinavyohitajika mwilini kuna kuhakikishia afya bora na hii itakusaidia sana kupunguza kuingiza kemikali nyingi mwilini unapokuwa unaumwa kwa kutumia dawa. Kinga ni bora kuliko tiba! Kula vyakula ambavyo vinaimarisha afya yako na si vinavyodumaza afya yako kama vyakula vyenye mafuta mengi na vyakula vilivyokoborewa.
Mboga hii inaweza kuliwa kwa chakula chochote; iwe ugali, wali, inaweza pia kutumika kungenezea juisi nzito (smoothie) Ni nzuri pia kutengezea kachumbari, supu ya mbogamboga. Uamzi ni wako tu ni kitu gani unapenda