Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Taarifa za awali zilipendekeza kunywa glasi nane(8) za maji kwa siku na taarifa bhizi hazikuwa na ushahidi wa kisayansi kwanini tufanye hivyo lakini ilikua ni muongozo tuu wa afya njema. Kutokana na hali halisi hata kama huzihitaji hizo glasi 8, huna budi kunywa maji ya kutosha kwa sababu ya faida zake muhimu sana mwilini :-
 
Kuwianisha kiwango cha vimiminika(fluids) ndani ya mwili.

-Asilimia kubwa (60%) ya mwili wa binadamu imeundwa na maji. Kazi ya vimiminika hivi mwilini ni pamoja na kusaidia mmeng’enyo wa chakula, mfumo wa damu, kutengeneza mate, usafirishaji wa virutubisho na kuchunga joto la mwili.
 
Kupunguza mwili/unene.

Kuchagua kunywa maji au vyakula vyenye wingi wa maji(mf. Matunda, mboga mboga, maharagwe n.k) badala ya vinyajwi vyenye calories nyingi au chakula chenye uelekeo huo ni chaguo sahihi kwani vinakufanya usihishi njaa kwakua ufyonzaji wake huenda kwa kasi ndogo.
 
Kupunguza mwili/unene.

Kuchagua kunywa maji au vyakula vyenye wingi wa maji(mf. Matunda, mboga mboga, maharagwe n.k) badala ya vinyajwi vyenye calories nyingi au chakula chenye uelekeo huo ni chaguo sahihi kwani vinakufanya usihishi njaa kwakua ufyonzaji wake huenda kwa kasi ndogo.
 
Kujenga na kuimarisha misuli.

Chembe chembe hai ambazo zinashindwa kuweka uwiano mzuri wa vimiminika ndani yake hupelekea misuli kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha na hivyo kuleta udhohofu wa mwili kwa ujumla.
Unywaji wa vimiminika kwa wingi ni muhimu wakati wa mazoezi ukifuata maelekezo vizuri kwani itasaidia upumuaji.
 
Afya bora ya ngozi na muonekano.

Ngozi yetu ina kiwango kibwa cha maji ambayo hufanya kazi ya kukinga upotevu mkubwa wa maji. Upotevu wa maji(Dehydration) hufanya ngozi iwe kavu sana na kupelekea uwe na mikunjo na makunyanzo katika ngozi ambayo huweza kuondoka kwa kupata kiwango sahihi cha maji.
 
Kusaidia figo.

vimiminika mwilini husafirisha taka mwili nje na ndani ya chembe hai. Taka kuu ndani ya mwili ni “blood nitrogen urea” ambayo huyeyuka ndani na maji na kupita kwenye mchujo wa mwili hivyo kutoka kwa njia ya haja ndogo.
Kiwango kidogo cha maji mwilini hupelekea kupata “kidney stones” hasa wakati wa joto kali.
 
*Madaktari wametoa tahadhari kuwa maambukizi ya COVID-19 yanaweza kuongezeka hasa kipindi hiki ambacho washabiki wa SIMBA FC wamekuwa wakiongea kwa nguvu na kurusha matemate kwa watu wengine, chukua tahadhari mapema kwa kujiepusha kwenda vijiwe vya mashabiki hao. Asante.*
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…