Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

:Mwaka 1956 Ateya alichaguliwa kama ofsa wa kwanza katika jeshi la ukombozi nchini misri .Wakati akitumikia jeshi alishiriki katika vita vya mgogolo wa mfereji wa SUEZ ambao ulivamiwa na umoja wa ulaya,ufaransa na Israeel .Katika vita hivo akiwafunza wanawake 4,000 namna ya kutoa huduma ya kwanza na masuala ya nursing Ni kutokana na uwezo wake katika vita mnamo july 14 mwaka 1957 alitumia kigezo cha uwezo wake katika vita kwenye kampeni zake za ubunge na kufanikiwa kuchaguliwa Ateya ndio mwanamke wa kwanza kuwa ofisa wa jeshi nchini misri na wa kwanza kuwa mbunge nchini humo na mwanamke wa kwanza katika nchi za kiarabu kuwa mbunge
 
:Sayari ya pluto inaukubwa wa eneo karibu nusu ya ukubwa wa marekani na kuifanya kuwa sayari ndogo zaidi katika mfumo wa Jua. Upo umbali wa milles billion 3.6 kutoka kwenye jua na ina miezi mitano(5 moons) .Charon ndio mwezi mkubwa zaidi katika mfumo wa jua ambao upo katika sayari ya pluto NASA walifanikiwa kufika katika sayari hii mnamo july 14 mwaka 2015 .
 
Dr Jane Goodall(86) ni moja ya watu wenye mchango mkubwa sana katika sekta ya utali Tanzania na sayansi ya wanyama duniani hasa Sokwe Mnamo July 14 mwaka 1960 akiwa hana elimu yoyote alifika katika hifadhi ya taifa ya Gombe ambapo aliishi porini kwa muda wa miaka 3 akiwa na sokwe akifanya utafiti wake .Jane amefanya utafiti wa sokwe kwa muda wa miaka 40 katika mbuga hiyo na miaka 60 katika kazi hiyo Ndiye mwanzilishi wa taasisi ya Dr Jane Goodall pamoja na Roots and Shoots ambayo ipo katika nchi 140 na wanachama zaidi ya 150,000 Utafiti huu wa Dkt Jane Goodall ulisaidia kubadilisha namna ambavyo sayansi iliwatambua sokwe na wanyama wengine na jukumu letu kama binadamu katika kujali kuhusu dunia yetu sote. Hapo awali, sayansi iliamini kwamba kilichotofautisha binadamu na sokwe ni uwezo wa kutengeneza zana, ingawa kwa utafiti wake huu, ulithibitisha kuwa sokwe nao hutengeneza zana zinazoendana na mahitaji yao ya kila siku. Pamoja na ugunduzi huo, pia Dkt. Goodall aligundua tabia nyingi za sokwe, ikiwamo uwezo wao wa kupanga kwaajili ya baadaye, kuona huruma, wivu, huzuni na kadhalika. Baada ya kukamilisha utafiti wake wa awali, Jane alirudi Uingereza na kuendelea na masomo ambapo alihitimu Shahada ya Uzamivu mwaka 1966 na kurudi Tanzania kuendelea kufanya shughuli zake za Utafiti kwenye hifadhi ya Taifa ya Gombe Ni utafiti huu ambao umemfanya Dkt. Jane Goodall kutambulika duniani kote, ikiwamo kupewa ubalozi wa amani na Umoja wa Mataifa, kupewa Shahada za heshima 42 na tuzo zaidi ya 107 na kupata uanachama kwenye taasisi kubwa zaidi ya 10 duniani kote kwa mujibu wa tovuti yake. Jane Goodall pia amekuwa alama muhimu ya amani duniani, huku wanaekolojia, wanasayansi na wanamazingira wakimpigia chepuo wakiamini anastahili Nobel Peace Prize
 
ABUNUASI . Moja ya Upekee wa mbuga zetu za Taifa Tanzania kama vile SERENGETI na nyinginezo ni kwamba unaweza ukaona wanyama ambao hukuwahi kujua au kutarajia kama wapo, . Ukiambiwa neno Abunuasii kichwani lazima itakuja picha ya binadamu flani hivi mwenye tabia fulani fulani 😃 (hii wahenga wanatumia sana, ukiwafunga kamba kidogo (uongo) au kupiga stori fulani ya kufikirika lazima wakwambie ACHA STORI ZA BUNUASII 😃😃) . Sasa Abunuasi mwenyewe halisi ni mnyamaa anayepatikana Serengeti, .anakichwa na masikio kama sungura lakini anamuonekano kama wa kangaroo, yaani miguu ya mbele ni miduuchu na miguu ya nyuma ni mirefu sana hivyo siku zote hutembea kwa kuruka ruka na miguu ya nyuma tu .kwa lugha iliyokuja na meli (ngeli) tunamwita SPRING HARE . Baadhi ya tabia zake, hupenda sana kulala hasa muda wa mchana na inapofika usiku ndipo huanza mishe mishe, (wanyama wengi wanaokuwa active night ni wale wazee wa vitongaa yaani kula kwa ulainii, hukamata wenzao wakiwa wamepiga mbonji😃) . Chakula chake kikuu ni majani na wadudu, .ni mnyama asiyeishi kijamii, na huweka makazi yake kwenye mashimo madogo na majani mafupi mafupi . Adui yake mkubwa ni nyani, maana nyani humlia timing kali sana bunuasi hasa ila mida anayoamka. kawaida jike hushika mimba kwa siku 77- 83 na huzaa watoto wawili .
 
ABUNUASI . Moja ya Upekee wa mbuga zetu za Taifa Tanzania kama vile SERENGETI na nyinginezo ni kwamba unaweza ukaona wanyama ambao hukuwahi kujua au kutarajia kama wapo, . Ukiambiwa neno Abunuasii kichwani lazima itakuja picha ya binadamu flani hivi mwenye tabia fulani fulani (hii wahenga wanatumia sana, ukiwafunga kamba kidogo (uongo) au kupiga stori fulani ya kufikirika lazima wakwambie ACHA STORI ZA BUNUASI) . Sasa Abunuasi mwenyewe halisi ni mnyamaa anayepatikana Serengeti, .anakichwa na masikio kama sungura lakini anamuonekano kama wa kangaroo, yaani miguu ya mbele ni miduuchu na miguu ya nyuma ni mirefu sana hivyo siku zote hutembea kwa kuruka ruka na miguu ya nyuma tu .kwa lugha iliyokuja na meli (ngeli) tunamwita SPRING HARE . Baadhi ya tabia zake, hupenda sana kulala hasa muda wa mchana na inapofika usiku ndipo huanza mishe mishe, (wanyama wengi wanaokuwa active night ni wale wazee wa vitongaa yaani kula kwa ulainii, hukamata wenzao wakiwa wamepiga mbonji . Chakula chake kikuu ni majani na wadudu, .ni mnyama asiyeishi kijamii, na huweka makazi yake kwenye mashimo madogo na majani mafupi mafupi . Adui yake mkubwa ni nyani, maana nyani humlia timing kali sana bunuasi hasa ila mida anayoamka. kawaida jike hushika mimba kwa siku 77- 83 na huzaa watoto wawili .
 
:Katika utafiti ulio fanywa na Swiss umeonyesha kuwa mtu mmoja kati ya watu 20 wenye furaha hufariki kutokana na furaha ya kupindukia Siyo habari au matukio mabaya tu ndiyo yanaweza kuleta athari kwenye afya ya mtu,hata kusababisha kifo. Habari nzuri pia zinaweza kusababisha mshituko wa moyo,hasa zinapotolewa kwa kushitukiza. Kama tunavyochukua tahadhari katika uwasilishaji wa taarifa mbaya kwa watu,tuwe na utaratibu pia wa kutafuta namna bora ya kuwasilisha taarifa bila kujali ni nzuri kiasi gani. Inaweza kuwa hatari pia
 
:Oktoba 3, 2014 mitandao ya Daily Mail, Metro na Fox News ilichapisha taarifa ya mwanamke wa umri wa miaka 22 raia wa Honda, Colombia aliyefika hospitali baada ya kulalamika maumivu ya kiuno na kukutwa na mizizi ya kiazi mviringo iliyoanza kuota ndani ya uke. Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina alisema alishauriwa na mama yake aanze kutumia njia za kuzuia ujauzito, ni kweli akaanza kutumia njia hizo alizoelezwa na mama yake ambazo moja wapo aliambiwa ajiweke kiazi kitamu ukeni. Majuma kadhaa baadaye akaanza kupata maumivu makali ya nyonga na kiuno, baada ya kufikishwa hospitali akakutwa ana mizizi ya viazi imeanza kuota kwenye kiazi ukeni. "Mama yangu aliniambia kuwa ikiwa sikutaka kupata ujamzito, napaswa kuweka viazi huko, na nikamwamini, nikaweka." Baada ya kuondolewa mizizi hiyo alipona kabisa, na taarifa ya madokta walioanza kumlaumu mama huyo kwa ushauri mbaya kwa bintiye ilisema kuwa hakuna madhara yoyote aliyoyapata. . . .
 
:Sio kwamba tu mchezo huo wa ngumi wanawake walikuwa hawaruhusiwi bali hata wanawake wenyewe waliuogopa .Rena alitoa nywele zake na kisha akayabana matiti na akafanya mabadiriko ya uso kisha akajiunga na team ya mchezo huo wa ngumi Alikuwa ni mbadala wa team yaani kama wameshindwa yeye ndio alikuwa muokozi wa team yake ambapo katika pambano la medali aliweza kuisababishia ushindi mkubwa team yake na akapewa medali Baadae ilijulikana kuwa hakuwa mwanaume na akanyangwanywa hiyo medali ambapo alirudishiwa tena april 2009 kabla ya kifo chake mnamo novemba 21,2009 akiwa na miaka 71 . . .
 
:Taifa la Cuba linamtambua Hatuey kama shujaa wa taifa .Enzi za uhai wake alifanya shughuli za kiharakati katika kuwatetea watu wake .Lakini Juhudi zake ziligonga mwamba Feb 2,1512 pale yeye na kundi lake walipo kamatwa Hatuey hakujua masuala ya dini .Katika dakika zake za mwisho kabla ya kunyongwa aliambiwa awe mkristo ili aende mbinguni na wamsamehe lakini alikataa huku akisema ni vema aende kuzimu. Baada ya hapo akanyongwa hadharani . .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…