Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JamiiForums859156439.jpg
 
Karen Greenlee kutoka Marekani, Alikuwa ni mhalifu ambae alikuwa anasumbuliwa na tatizo kitalaam linaitwa "Necrophilia" ambayo humfanya mtu kutamani/Kufanya mapenzi na maiti. Mwaka 1979 alikamatwa baada ya kuiba maiti ya mzee mmoja na kwenda kufanya nayo mapenzi, Alitozwa faini Tsh 591,441 na kifungo cha siku 11 jela.
 
Magari yenye thamani ya juu zaidi kwa sasa;

1. Bugatti La Voiture Noire- Tzs Bilioni 44
2. Rolls-Royce Sweptail- Tzs Bilioni 30
3. Bugatti Centodieci- Tzs Bilioni 20
4. Mercedes-Benz Maybach Exelero- Tzs Bilioni 18
5. Koenigsegg CCXR Trevita- Tzs Bilioni 11
6. Lamborghini Veneno- Tzs Bilioni 10
7. Lamborghini Sian- Tzs Bilioni 8
8. V Motors Lykan Hypersport- Tzs Bilioni 7
9. Limited Edition Bugatti Veyron By Mastory Vivere- Tzs Bilioni 7
10. Ferrari Pinifarina Sergio- Tzs Bilioni 6.9
 
Inaelezwa kwamba matumizi makubwa ya vinywaji vya kuongeza nguvu (Energy Drinks) yanaweza kupelekea ugonjwa wa Homa Ya Ini, Ikihusishwa na tukio la mwaka 2016 la mzee wa miaka 50 aliyepatwa na ugonjwa huo huku chanzo ikielezwa ni matumizi makubwa ya Vinywaji hivyo. Kwa siku alikuwa anatumia kopo 4 mpaka 5.
 
Viktor Jasinski, Urusi alienda kuiba katika moja ya duka la nywele bandia, Alikamatwa na mmiliki wa Duka hilo ambae ni Mwanamke kisha kufungwa kwa siku 3 katika Chumba kidogo ndani ya Duka hilo kisha kutumikishwa kwa lazima kingono huku akisema alikuwa akipewa Viagra tu kwa siku zote hizo. Mmiliki wa Duka hilo alikuwa Mcheza Karate anaeshikilia mkanda mweusi.
 
Baadhi ya mateka baada ya muda hujenga mahusiano ya karibu na waliowateka na kuanza kuwahurumia. Hii imepewa jina la Stokholm Syndrome ambapo kwa mara ya kwanza ilishuhudiwa mwaka 1973, Sweden ambapo mateka waliwatetea watekaji wakati wa zoezi la uokozi.
 
Mama Joan Wicken, Muingereza, Alikuwa msaidizi wa Mwalimu Nyerere na Mwandishi wa Hotuba zake kwa miaka yote ya utawala wake hadi Mwl. Nyerere alipofariki mwaka 1999. Pamoja waliandika kitabu kinachotazamiwa kutoka mwaka 2029, Joan Wicken alifariki mwaka 2004.
 
Back
Top Bottom