Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukishanyunyizia mbolea ya kupandia ichanganye vizuri na udongo. Sia mbegu kwenye hiyo mifereji halafu funika kwa udongo. Kisha mwagilia mara kwa mara kadri mahitaji yanavyoongezeka. Hapa ina maana kwamba kadri mmea unavyokua ndivyo unahitaji maji mengi zaidi. Mimea ikashakua, punguza mimea, na uache sentimita 8 (cm) kati ya mmea na mmea. Ile mimea unayoipunguza inaweza kupandwa sehemu nyingine.Hivyo basi nafasi ya mimea itakua ni 30 X 8 cm. Yaani mstari hadi mstari ni sentimita 30 na nafasi ya mche hadi mche ni sentimita 8.
 
NJIA YA PILI: UPANDIKIZAJI WA MICHE (TRANSPLANTING).
Hapa Miche inakuzwa kwenye kitalu kwa wiki 6 hadi 8 tangu kisia mbegu kisha inahamishiwa shambani. Inakadiriwa kwamba wiki 6 hadi 8 miche itakua imefikia kiwango kizuri cha ukuaji kwa ajili ya kuhamishiwa kwenye shamba kuu (main field).
 
Hii ndio njia inayoshauriwa zaidi na ndiyo inayotumia na wakulima wengi wa vitunguu. Hapa Tanzania upandaji wa mbegu za vitunguu katika kitalu kwa ujumla huanza mwezi machi hadi mei kutegemea na msimu wa kilimo.
 
Hivyo kilimo hiki hufanyika mara baada ya mvua za masika kubwa kuisha. Kipindi cha kiangazi na baridi huruhusu ukuaji mzuri wa vitunguu. Mbegu za vitunguu huoteshwa mapema katika kitalu. Mbegu zinaweza kupandwa kwa mstari au kwa kutawanya katika tuta la kitalu. Katika upandaji wa mstari, mbegu hupandwa katika nafasi ya cm 10 hadi 15 kati ya mstari na mstari.
 
Baada ya kupanda, mbegu hufunikwa kwa udongo na baadaye kwa kuweka matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu kuota, matandazo yaondolewe na badala yake kichanja cha nyasi kijengwe ili kuiwekea kivuli mimea michanga. Mbegu huota baada ya siku 7 hadi 10.
 
JINSI YA KUKUZA MICHE VITUNGUU KWENYE KITALU
Tengeneza matuta yaliyoinuka (raised seed beds) yenye upana wa mita 1 na urefu utakaopenda. Urefu mzuri wa tuta unaweza kuanzia mita 2 hadi 5. Idadi ya matututa itategemea na wingi wa mbegu unazotaka kusia. Weka Mbolea ya samadi iliyooza vizuri. Itawanye vizuri kwenye matuta ya kitalu Weka Mbolea ya kupandia ya viwandani kama TSP au MAP.
 
Kisha changanya vizuri na udongo. Hakikisha Samadi, mbolea ya ya Kupandia TSP vyote vinachanganyika vizuri kwenye udongo. Tengeneza mistari ambayo iko kama mifereji midogo yenye urefu wa sentimita 2. Mistari hiyo iwe umbali wa sentimita 5 kutoka mstari hadi mstari.Sia mbegu za vitunguu kwenye mistari hiyo kisha funika na udongo kidogo. Funika tuta lako kwa nyasi zilizokauka. Nyasi zinasaidia kutunza unyevunyevu wa udongo pamoja na joto la udongo litakalosaidia miche kuota vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…