Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama ni msimu wa jua kali, tengeneza kichanja ambacho juu yake utafunika na nyasi chache ili kupunguza ukali wa mionzi ya jua kwenye miche. Kila tuta unaweza kulijengea kichanja chake. . Hakikisha kitalu hakina magugu wakati wote, kwa maana vitunguu vina mizizi mifupi (shallow roots) na haiwezi kushindana na magugu.Pandikiza miche yako kwenye shamba kuu mara miche inapofikia urefu wa sentimita 15.
 
UPANDIKIZAJI WA VITUNGUU.
Vitunguu vinapsawa kupandikizwa wakati wa asubuhi au au jioni. Wakati wa jioni ndio mzuri zaidi wa kuhapandikiza miche. Miche inapaswa kupandwa kina kilekile kama ilivyokua kwenye kitalu. Yaani mche unapong’olewa kwenye kitalu kuna sehemu ilikua chini ya ardhi.
 
Yaani urefu wa mstari na mstari uwe sentimita 30 na nafasi ya mche na mche iwe sentimita 8. Nafasi inaweza kutoafutiana kidogo kulingana na aina ya mbegu, lakini pia kulingana na ukubwa wa kitunguu unachotaka. Ukitaka vitunguu vikubwa, nafasi inaongezeka, yaani vinapandwa mbalimbali. Ukitaka vitunguu vidogo unapunguza nafasi, yaani unapanda karibukaribu.
 
Yaani urefu wa mstari na mstari uwe sentimita 30 na nafasi ya mche na mche iwe sentimita 8. Nafasi inaweza kutoafutiana kidogo kulingana na aina ya mbegu, lakini pia kulingana na ukubwa wa kitunguu unachotaka. Ukitaka vitunguu vikubwa, nafasi inaongezeka, yaani vinapandwa mbalimbali. Ukitaka vitunguu vidogo unapunguza nafasi, yaani unapanda karibukaribu.
 
KUNDI LA PILI: MBOLEA ZA KUKUZIA:
Mbolea hizi huwekwa kipindi cha ukuaji wa mmea (vegetative growth) na hua na lengo la kuupa mmea ukuaji mzuri utakaopelekea kua na majani mazuri yatakayotengeneza chakula cha kutosha cha kwenye mmea.

Kitendo hichi cha mmea kutengeneza chakula chake huitwa Photosynthesis na hufanyikia kwenye majani. Kirutubisho kikuu katika kundi hili la mbolea ni Nitrogen (N). Baadhi ya mbolea zilizopo kwenye kundi hili ni pamoja na UREA, SA, CAN n.k.

Pia kwenye kundi hili zipo mbolea za maji zinazopigwa kwenye majani (foliar fertilizers) hujulikana pia kama booster.
 
KUNDI LA TATU: MBOLEA ZA KUZALISHA/KUKOMAZIA KITUNGU.Hizi ni zile zinazowekwa kuusaidia mmea kutengeneza kitunguu (bulb formation). Kirutubisho kikuu hapa ni Potassium. Ili Kituunguu kiweze kujijenga vizuri na kua na ubora mzuri kinahitaji mbolea zenye kitutubisho cha Potassium. Mfano wa mbolea zenye virutubisho hichi ni Multi K, MOP (Muriate of Potash) n.k.Hayo ndio makundi makuu ya mbolea, japokua mbolea hizo hujumuisha pia virutubisho vidogo (micro nutrients) ambavyo vinahitajika kwa udogo kwenye mimea, japokua zina kazi muhimu kwenye mimea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…