Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

WADUDU WAHARIBIFU
Kuna aina tatu (3) za wadudu wanao haribu zao hili:
VIROBOTO WA VITUNGUU Hawa ni wadudu waharibifu namba moja wa zao la vitunguu hapa nchini Tanzania. Husababisha upotevu mkubwa wa mavuno. Wadudu hawa huonekana hasa wakati wa kipindi cha joto.
 
Ili kupunguza uvamizi mkubwa, panga upandaji wa vitunguu mapema ili kipindi cha joto kiingiapo zao lako liwe limekomaa. Epuka kupanda zao la vitunguu sehemu iliyo kuwa na mazao aina ya vitunguu kama vile liksi, vitunguu swaumu, n.k.
 
(Thrips) ambao wanashambulia majani, Uharibifu uletwao na wadudu chawa, unatofautiana msimu mmoja na mwingine kutegemeana na hali ya hewa. Mvua kidogo pamoja na joto kali unasababisha mlipuko wa wadudu. Wanashambulia majani kwa kukwarua kwarua na kunyonya maji hivyo kusababisha majani kuwa na rangi ya fedha/siliver na baadaye majani yanakauka.
 
SOTA (CUTWORMS) Sota au viwavi wa nondo wanasababisha uharibifu mkubwa. Viwavi wanakata mashina ya miche michanga sehemu ya chini ya shina juu ya ardhi. Sota wanapendelea kula wakati wa usiku na mchana kujificha kwenye ardhi karibu sana na sehemu waliokata shina. Uharibifu huu unapunguza sana idadi ya mimea shambani na kuleta upungufu wa mazao. Wadudu hawa wanadhibitiwa kwa kupulizia dawa kama; Karate Dursban na Actellic na kuweka shamba katika hali ya usafi.
 
UTITIRI WEKUNDU (RED SPIDER MITES) Hawa ni wadudu wadogo sana, ambao wanajificha upande wa chini wa majani. Wanafyonza maji kwenye majani na kusababisha majani kuwa na rangi nyeupe. Wadudu hawa wanatengeneza utando mweupe kuzunguka majani na mashina. Mmea unashindwa kutengeneza chakula na baadaye inakufa.Njia ya kudhibiti: Kupulizia dawa za wadudu Karate na Selecron. Kuteketeza masalia ya mazao Kutumia mzunguko wa mazao
 
Hizi dawa ni nzuri kwani zina uwezo wa kuua magugu aina mbalimbali. Dawa Inapuliziwa wiki mbili mpaka tatu baada ya kupandikizwa miche shambani. Palizi baada ya kutumia dawa ya magugu ni muhimu ili kuondoa magugu sugu na pia kutifulia vitunguu Wakati wa palizi, vitunguu na mizizi iliyowazi ifunikwe kwa udongo ili kuzuia jua lisiunguze mizizi au kubabua vitunguu.
 
UVUNAJI WA VITUNGUU
Muda wa ukomaaji wa vitungu hutegemea aina ya vitunguu pamoja na hali ya hewa ya eneo husika. Aina za chotora  (hybrid) mara nyingi hukomaa mapema, huchukua miezi 3 hadi 5 baada ya kusia mbegu. Aina za kawaida (OPV) na zile za kienyeji hazina ukomaaji unaofanana (do not mature uniformly), hukomaa kwa makundi makundi.
 
Yale majani ya nje yanayofunika kitunguu unene wake unapungua. Hizo ndio dalili za kitunguu kua tayari kwa kuvunwa. Uvunaji wa mapema (early harvest) hupelekea vitunguu ambavyo havijakomaa vizuri, hivyo kusababisha kupoteza maji na kusinyaa kwa vitunguu wakati wa ukaushaji wa vitunguu.
 
Pia uvunaji wa kuchelewa (late harvest) husabisha kitunguu kupoteza rangi yake, kuoza kwa yale maganda/majani yanayokua yamekifunika kitunguu chenyewe (onion bulb). Hivyo basi kitunguu kinapaswa kuvunwa kwa wakati sahihi ili kuepuka hasara inayoweza kutokana na kuwahi au kuchelewa katika uvunaji
 
Back
Top Bottom