Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji3][emoji3][emoji3]Wajumbe sio watu wazuri
 
Tembo ni mnyama wa nchi kavu jamii ya mamalia. Ndiye mnyama mkubwa kuliko wote waishio nchi kavu. Kuna aina mbili za tembo duniani, tembo wa bara la Afrika na tembo wa bara la Asia. Kuna spishi mbili za tembo wa Afrika; tembo wa msituni na tembo wa uoto wa savana. Tanzania ina tembo wa savana pekee. Tembo wa msituni hupatikana katika nchi za Afrika ya Kati na Magharibi.
 
Tembo anakadiriwa kuwa na uzito wa kilo 6600 (tani 6.6) kwa madume na kilo 3300 (tani 3.3) kwa majike. Tembo huishi miaka 60 hadi 70. Tembo hupendelea kula mimea, magome ya miti, matunda,majani na nyasi. Kuna tofauti kati ya tembo dume na tembo jike. Tembo dume huwa na mwili mkubwa uliojengeka, paji la uso huwa na mviringo lakini tembo jike huwa na paji lililochongoka.
 
Faida za tembo kiuchumi;

Hapa nchini, kwa zaidi ya asilimia 90 ya utalii unategemea wanyamapori. Watalii wengi huja kuwaona wanyama, kuwapiga picha na kuondoka. Wanyamapori wamebeba utalii kwa kiasi kikubwa na utalii umesaidia kukuza uchumi wa nchi hii – Wanyama hawa kupitia utalii wanasaidia kupata fedha za dawa, vitabu mashuleni, wanatujengea barabarana miundo mbinu nyingine na pia wanalipa mishahara kwa watumishi wa umma.
 
Huchangia patika pato la taifa. Tembo pamoja na wanyamapori wengine wamekua kivutio kikubwa cha utalii hivyo hutusaidia kupata hata fedha za kigeni ambazo husaidia maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu. Mfano sekta ya utalii kwa mwaka 2016 ilichangia 17.5% ya pato la taifa na 25% ya fedha za kigeni.
 
Chanzo cha ajira. Uwepo wa tembo na wanyama wengine umepelekea watu wengi kuajiriwa katika sekta ya wanyamapori na utalii. Kwa mfano mwaka 2016, watu takriban 600,000 waliajiriwa moja kwa moja katika sekta ya utalii na wengine takriban milioni moja katika ajira mbadala
 
Ni kivutio cha watalii. Tembo ni mnyama ambaye ana mvuto sana kutokana na ukubwa, uzuri wake wa asili na muundo wa jamii na tabia yake. Takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha kuwa watalii waliotembelea Tanzania walikua 1.284,279 ambao ni ongezeko la 12.9% ukilinganisha na mwaka 2015 ambao watalii waliofika Tanzania walikua milioni 1,137,182.
 
Faida Za tembo kitamaduni:

Tembo ni urithi wa Taifa letu. Tembo ana umuhimu sana katika utamaduni wa kiafrika. Kwa mfano, hutokea katika mapambo kama vile hereni, pete na hata michoro ya kwenye mavazi. Pia tembo wana nafasi maalumu katika hadithi za kiafrika. Hivyo tembo, kama wanyama wengine ni urithi wa taifa letu.
 
Faida za tembo kimazingira.

Tembo ni mnyama tegemeo kwa wanyama wengine na muhimili mkubwa katika mfumo wa ikolojia. Mfano, wakati wa kiangazi tembo hutumia meno yao kuchimba maji ardhini, hii huwawezesha tembo kuishi katika mazingira kame. Maji hayo huwafaidisha wanyama wengine wakubwa na wadogo. Pia wakati wa kiangazi tembo huangusha matawi makubwa ya miti ambayo huwawezesha wanyama wadogo kupata chakula mfano swala, pundamilia na hebivora wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…