Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tembo husaidia kusafisha na kutengeneza mazingira ya mbuga. Tembo wasingekuepo, mazingira ya savana yangeonekana tofauti sana. Tembo hula mimea na vichaka vya miti ambapo hufungua misitu na mapori kuwa mbuga wazi kutoa nafasi kwa mimea mengine kuota na njia kwa wanyama wengine.
 
Tembo husaidia kuongezeka kwa idadi ya mimea. Hii ni kutokana na ulaji wao wa mimea yenye mchanganyiko wa mbegu mbalimbali. Popote wanapoishi huacha kinyesi kilichojaa mbegu. Mbegu hizi huchipua na kuwa nyasi, miti na hata misitu hivyo husaidia kuongezeka kwa mimea na afya ya mazingira kwa ujumla
 
Kinyesi cha tembo ni chanzo cha chakula kwa wanyama kama tumbili, ndege na nyani. Pia kuna wadudu hutegemea kinyesi cha tembo kama chakula mfano mende kibyongo (dung beetle). Kinyesi cha tembo pia ni chanzo cha rutuba katika udongo hivyo kuongeza afya ya mazingira.
 
Pamoja na faida nyingi za tembo, kuna changamoto nyingi zinazomkabili mnyama huyu mfano ujangili na migogoro baina yao na binadamu. Ujangili umeongezeka kutokana na uwepo wa biashara ya meno ya tembo katika masoko ya bara la Asia. Serikali inapaswa kuunga mkono jitihada za kimataifa za kuikakabili biashara hii kwani kuna mataifa tayari wameshaonyesha nia ya kufunga masoko kwa mfano China.
 
Jukumu la kuzuia ujangili si la serikali pekee. Dhana hii ni potofu kabisa kwani, uzuiaji ujangili kamwe hautafanikiwa kama wananchi na wadau wengine walioko ndani na nje ya nchi yetu wataendelea kubakia watazamaji tu. Ni muhimu kila mwananchi mzalendo wa nchi hii ashiriki kikamilifu katika ulinzi wa nchi na rasilimali zake zote kama katiba ya nchi inavyotuasa.
 
IMG_20200724_082033.jpg
 
Back
Top Bottom