Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Binadamu tunafanya maamuzi na viumbe wengine pia wamepewa uwezo wa kufanya maamuzi ingawa tofauti ya maamuzi ya watu na viumbe vingine ni kwamba wakiwa na ufahamu watu wanaweza kuchagua cha kuamua,lakini wanyama au viumbe wengine wanaamua bila kujua kwa sababu wamenyimwa uwezo muhimu unaitwa ufahamu.
 
Wakati mwingine tumefanya maamuzi katika maisha yetu na kupata matokeo mabaya na mwisho wake kuishia kulaumu watu au kuweka visingizio vya kwa nini tumeshindwa kupata matokeo mazuri.Hapa mara nyingi tumeshindwa kujilaumu na kusukumiza lawama kwa watu wengine.
 
Maamuzi tunayofanya yapo ambayo yataleta matokeo ya kutufanya tuheshimike katika jamii na yapo yale ambayo yanatufedhehesha hata sisi wenyewe na katika jamii inayotuzunguka. Mimi na wewe jinsi tulivyo leo ni matokeo ya maamuzi tuliyowahi kufanya wakati fulani.
 
Hujawahi kufanya uamuzi katika maisha yako ambapo umeendelea kujuta kila unapoona matokeo yake japokuwa ni miaka mingi sasa imepita tangu ufanye uamuzi? Wakati unapotamani siku zingeweza kurudi nyuma ukatafakari upya na kufanya uamuzi mzuri usiozaa majuto siku za usoni.
 
Kwa mfano mama mmoja aliyekuwa na ndoa yake nzuri aliamua kusikiliza ushauri wa shoga yake kutokutulia ndani ya nyumba naye akaamua kutekeleza hivyo hivyo na matokeo yake akapewa talaka,dunia ilikuwa inamlaumu huyo mwanamke haikumlaumu aliyemshauri.
 
Nataka nikukumbushe tu kwamba hakuna wa kumsingizia unao uwezo ndani yako wa kufanya kitu chochote,wakati wowote na kikawa.Unao uwezo wa kuamua sasa kurudi shule na kuwa miongoni mwa wanafunzi bora,unao uwezo wa kuanzisha biashara na ikawa,unao uwezo wa kuamua sasa hivi kuwa na mawazo na matokeo chanya na ikawa,unao uwezo wa kuamua sasa kuoa au kuolewa na ikawa,unao uwezo wa kuamua kuanza kujenga na ukawa,unao uwezo wa kuamua maisha yako kuanza kugusa maisha ya watu wengine na ikawa,unao uwezo wa kuamua kuanza kutumia vipaji Mungu alivyoweka ndani mwako kwa ajili ya maisha ya watu wengine na ikawa. Hakuna cha kukusimamisha.
 
Kama umesoma unamiliki cheti chako kizuri lakini bado hujapata kazi na hakuna kitu chochote unachofanya eti kwa sababu hujapata kile unachokiita ajira,tafsiri yake ni kwamba maisha yatakuwa magumu,utalaumu watu kila siku kwa sababu tayari umekwishafanya uamuzi wa kukaa tu.
 
Ingawa watu wote wanafanya maamuzi kila saa ni kitu gani kinachotofautisha mtu mmoja na mwingine? Uamuzi ni wazo lililo ndani ya fikra za mtu na mtu ana uwezo wa kuamua kubaki na uamuzi wake mwenyewe bila kufanya kitu chochote.Kitu kinachotutofautisha watu sasa ni matendo.
 
Ili uamuzi uweze kuwa na maana lazima sasa uamuzi huo uusukume kuwa katika hatua ya matendo. Matendo yanaweza kuwa makubwa,wastani au madogo na matokeo yake yatakuwa vivyo hivyo. Matendo ni kichocheo kikubwa cha maamuzi na ndicho chanzo cha matokeo mazuri na mabaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…