Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuwa mwangalifu sana na maamuzi yako kwani umepewa uwezo wa kumiliki mwenyewe na utawajibika kwa matokeo mazuri au mabaya ya maamuzi yako wewe mwenyewe.Jinsi ulivyo,hali uliyo nayo ni matokeo ya umauzi uliyowahi kufanya wakati fulani.
 
Umewahi kukutana na mtu anadai kufanya kila kitu kwa mafanikio? Hakuna kitu au kazi maalum ambayo inaweza kumtambulisha mtu huyo maana anafanya kila kitu kinachokuja mbele yake. Anachangamkia kila fursa na kuhudhuria kila semina ya ujasiliamali inayokuja mbele yake.Leo nataka tupite kwenye mada ambayo nimeipa kiwachwa “HATUKUUMBWA KUFANYA KILA KITU”.
 
Kwa kukosa maarifa sahihi watu wengi wanaishi wakidhani kuwa mtu anaweza kufanya kila kitu na kufanikiwa katika mambo yote anayotia mkono lah! hasha! Siyo kweli hukuumbwa kufanya kila kitu kipo kitu maalum ambacho wewe upo kwa ajili ya kukifanya kitu hicho hata kama ni kimoja tu.
 
Watu wengi waliofanikiwa na kupata umaarufu ni kwa sababu walitambua na kuchagua kitu kimoja cha kufanya katika maisha yao yote,na hicho kitu kimoja walichofanya kimewafanya kujulikana na kuwafikisha kwenye mafanikio makubwa pia.
 
Huwezi kwa mfano kuwa bingwa katika michezo yote,yaani wewe uwe bingwa mieleka,wakati huo huo uwe bingwa wa mchezo wa ngumi,mchezo wa kuogelea n.k haiwezekani kuwa bingwa katika kila eneo na ndiyo maana unakuta hata katika taaluma kuna madaktari bingwa kwa mfano magonjwa ya wanawake,watoto,kichwa,mfumo wa hewa huwezi kukuta daktari bingwa katika kila eneo haiwezekani. Hata kama kwa sehemu anajua maeneo mengine kwa maarifa ya msingi lakini lazima liwepo eneo ambalo amebobea kuliko maeneo mengine.
 
Daktari akishindwa kuchagua na kujielekeza kwenye eneo moja basi wanaomsimamia kupata huo ubingwa hawawezi kabisa kumpitisha mtu huyo kuwa ni bingwa katika eneo fulani la taaluma kwa sababu ameshindwa kuchagua na kujielekeza katika eneo moja kwa hiyo hawezi kuwa bingwa wa eneo lolote.
 
Hatukuumbwa kufanya kila kitu,narudia tena si mpango wa Mungu binadamu kufanya kila kitu ndipo aishi kwa mafanikio makubwa.Unaweza kuwa na kitu kimoja tu ambacho utaambatana nacho katika maisha yako yote na mwisho wa siku dunia itakutambua kwa hicho ulichoamua kufanya kwa muda mrefu.
 
Tafsiri ya mtu kufanya kila kitu kwa lugha nyepesi ni mtu kukosa kujua na kutambua kusudi la kuwepo kwake hapa duniani. Mtu yeyoyote anaejua kile alichoitiwa kuja kufanya hapa duniani hawezi kuishi kwa kufanya kila kitu kinachokuja mbele yake hata kama watu walio karibu naye wanamwona kwamba anaweza kufanya kila kitu,lazima ataishi kile anachosikia moyoni kwa sababu maisha ni yake binafsi haishi kwa ajili ya mtu mwingine.
 
Kwa hiyo kama unataka kuanza kuishi maisha ya kifuatilia kitu au vitu vichache katika maisha basi unapaswa kuanza kutafuta msaada watu wakusaidie maarifa ya namna ya kutambua na kujua kusudi la kuwepo kwako duniani ili uanze kuliishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…