Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Erasto Mpemba akiwa mwanafunzi wa kidato cha 3 mwaka 1963 katika Shule ya Sekondari Magamba alifanya jaribio na kugundua maji ya moto yanaganda haraka zaidi kuliko ya baridi. Mara ya kwanza wakati anaelezea darasani alichekwa na wenzake, Lakini Profesa Osborne kutoka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam alikuja kuthibitisha hilo mwaka 1969. Jaribio hilo lilipewa jina la Mpemba Effect na linakubalika Dunia nzima.
 
KATIKA MIAKA YA 1930 HAD MWISHONI MWA MIAKA YA 1940 SUNGURA ALIKUWA ANATUMIKA KAMA KIPIMO CHA MIMBA

Mkojo wa mwanamke mwenye mimba unaingizwa kwenye sindano kisha anachomwa nayo sungura

Kama sungura atabaki hai huyo nwanamke hana mimba

Ila kama sungura akifa basi huyo mwanamke ana mimba
 
UKIPATA CORONA UTALIPWA DOLA ELFU 3 ZA KIMAREKANI nchini Uzbekistan

Nchi ya Uzbekistan imetangaza kuwa itamlipa mtu yoyote yule atakaekwenda kutembea nchi hiyo halafu akapata korona

Lengo hilo la kutangaza dili hilo ni kwa ajili ya kutangaza na kuimarisha sekta yao ya utalii ambayo imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mlipuko wa gonjwa la corona

Dola za kimarekani elfu 3 ambazo ni zaidi ya million 6 za kitanzania
Hiyo yote ni kutaka kuwaaminisha watalii kuwa nchi hiyo ni salama kwa sasa na serikali imechukua hatua zote katika kuhakikisha usalama kwa watalii wote

Ukumbuke kwa mwaka 2019 Uzbekistan ilikuwa ni nchi ya nne kwa uchumi wake kukuwa kwa haraka
 
ndio ni Vita kati ya Ugiriki na Bulgaria mwaka 1925

Wanajeshi waliopo katika eneo la Petrich ambalo ni eneo la mpaka kati ya nchi ya Ugiriki na Bulgaria ndio walihusika katika Vita hivyo

Mwanzoni mwa mwezi wa 10 katika mwaka 1925 mwanajeshi wa Ugiriki alipigwa risasi na wanajeshi wa Bulgaria baada ya kuvuka mpaka wa nchi yake na kuingia nchi ya Bulgaria wakati anafukuza mbwa wake

Kuuliwa kwa mwanajeshi wa kigiriki kulizua hasira kwa wanajeshi wenzake hivyo nao wakaamua kuivamia Bulgaria kwa na kushikilia vijiji kadhaa vya Bulgaria vilivyopo mpakani

Baadae Umoja wa mataifa wa wakati huo (league of nations) waliingilia Kati na kutatua changamoto hiyo

Lakini hadi league of nations anakuja kusawazisha watu zaidi ya 50 walikuwa tayari wameshafariki dunia

Kama asingekuwa mbwa kukimbia basi haya yote yasingetokea
 
Back
Top Bottom