Inaelezwa kwamba muuzaji nguli wa Madawa Ya Kulevya, Pablo Escobar alikuwa anatumia Tsh Milioni 5.8 kila mwezi kwaajili ya kununua raba za kufungia pesa zake
Kimo chako kina mchango katika kuongeza au kupunguza muda ambao utajifungua mtoto (Labor), Mwanamke mrefu huchukua muda mrefu zaidi kujifungua tofauti na mfupi.
Erasto Mpemba akiwa mwanafunzi wa kidato cha 3 mwaka 1963 katika Shule ya Sekondari Magamba alifanya jaribio na kugundua maji ya moto yanaganda haraka zaidi kuliko ya baridi. Mara ya kwanza wakati anaelezea darasani alichekwa na wenzake, Lakini Profesa Osborne kutoka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam alikuja kuthibitisha hilo mwaka 1969. Jaribio hilo lilipewa jina la Mpemba Effect na linakubalika Dunia nzima.
Katikati ya Mapanga ya Helikopta kuna nati inaitwa "Jesus Nut" kazi yake kuu ni kushikilia mapanga yote. Imepewa jina hilo kwa sababu ikifeli kitachofuata ni sali Mungu akusaidie utoke salama.
Zana, Ni mwanamke aliyeishi Urusi miaka ya 1850. Alikamatwa porini akiwa na muonekano wa kila kitu kama Sokwe na kufugwa. Baadae alianza kubadilika muonekano kuwa kama binadamu, Alizaa watoto na kizazi chake kipo hadi sasa.
Jiji la Doha nchini Qatar ndio jiji la kwanza kuwa na barabara za rangi ya blue
Lengo la kubuni aina hizo za barabara ni kutaka kupunguza kiwango cha joto kwenye barabara ambacho kinakadiriwa kufikia nyuzi 15 hadi 20
UKIPATA CORONA UTALIPWA DOLA ELFU 3 ZA KIMAREKANI nchini Uzbekistan
Nchi ya Uzbekistan imetangaza kuwa itamlipa mtu yoyote yule atakaekwenda kutembea nchi hiyo halafu akapata korona
Lengo hilo la kutangaza dili hilo ni kwa ajili ya kutangaza na kuimarisha sekta yao ya utalii ambayo imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mlipuko wa gonjwa la corona
Dola za kimarekani elfu 3 ambazo ni zaidi ya million 6 za kitanzania
Hiyo yote ni kutaka kuwaaminisha watalii kuwa nchi hiyo ni salama kwa sasa na serikali imechukua hatua zote katika kuhakikisha usalama kwa watalii wote
Ukumbuke kwa mwaka 2019 Uzbekistan ilikuwa ni nchi ya nne kwa uchumi wake kukuwa kwa haraka
ndio ni Vita kati ya Ugiriki na Bulgaria mwaka 1925
Wanajeshi waliopo katika eneo la Petrich ambalo ni eneo la mpaka kati ya nchi ya Ugiriki na Bulgaria ndio walihusika katika Vita hivyo
Mwanzoni mwa mwezi wa 10 katika mwaka 1925 mwanajeshi wa Ugiriki alipigwa risasi na wanajeshi wa Bulgaria baada ya kuvuka mpaka wa nchi yake na kuingia nchi ya Bulgaria wakati anafukuza mbwa wake
Kuuliwa kwa mwanajeshi wa kigiriki kulizua hasira kwa wanajeshi wenzake hivyo nao wakaamua kuivamia Bulgaria kwa na kushikilia vijiji kadhaa vya Bulgaria vilivyopo mpakani
Baadae Umoja wa mataifa wa wakati huo (league of nations) waliingilia Kati na kutatua changamoto hiyo
Lakini hadi league of nations anakuja kusawazisha watu zaidi ya 50 walikuwa tayari wameshafariki dunia
Kama asingekuwa mbwa kukimbia basi haya yote yasingetokea
Wanaanga wa Marekani Doug Hurley na Bob Behnken wamekiondoa chombo chao ndani ya mtambo wa kuondokea kutoka kituo cha anga za mbali kwa ajili ya kuanza safari yao ya kurejea duniani.
Wawili hao wanatawajiwa kutua ndani ya maji kwenye eneo la mwambao wa Florida nchini Marekani muda mfupi baada ya saa nane za dakika aroibaini na tano 14:45 kwa saa za Marekani leo Jumapili.
Kutua salama kwa chombo hicho kutamaanisha kwamba Marekani kwa mara nyingine tena ina uwezo wa kuhudumu, ina kibali kamili cha watu wake kuweza kuingia katika uzio wa dunia na anga za mbali na kurejea duniani.