Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

DOUBLE AGENTS NGULI WANNE KUWAHI KUTOKEA KATIKA ULIMWENGU WA UJASUSI

Mustakabali wa taifa lolote lile hutegemea pamoja na mambo mengine mifumo ya ulinzi, kwani hii ndio nguzo mhimu katika kuhakikisha ustawi wa maslahi ya taifa husika

Ni kwa msingi huo basi mataifa yote duniani yameunda vyombo tofauti tofauti vya ulinzi mojawapo ikiwemo idara za ujajusi, mifano ipo mingi, CIA, M16, BND, MOSSAD, TISS n.k!

Lakini kuwa na taasisi au vyombo hivyo vinahiyaji nguvu kazi, nguvu kazi hii sharti iwe yenye weledi na uzalendo wa kutukuka, kwani kazi wanayoifanya ni kazi nyeti mno na inayozungukwa na mambo mengi sana, hivyo kuteleza kwa namna yoyote ile basi kunaacha madhara makubwa mno! Na kiukweli wapo walioteleza na kuleta madhara yasiyoelezeka, sasa Leo nimeona tuangalie kwa ufupi baadhi ya wanausalama walioteleza na kujikuta walitumia pande mbili au zaidi maarufu kwa jina la *DOUBLE AGENT*
 
Lakini kwanza kabisa double agent ni nani?*

Tunaweza tukasema ni afisa usalama wa tasisis au serikali ambaye amepewa majukumuu ya kuichunguza taasisi au nchi nyingine lakini wakati huo huo anakuwa tena anafanya kazi hiyo hiyo kwa ajiri ya taasisi au nchi anayopaswa kuichunguza dhidi ya taasisi au nchi iliyomtuma! Wengi wanasem double agent anaweza kuwa matokeo ya tamaa ya pesa, kulazimishwa( baada ya kutishiwa kufanyiwa kitu kibaya), mapenzi tu, yaani mtu anapenda tu kuwa double agent, kupandikizwa kwa makusudi( marekani wamefaidika sana na aina hii hasa Mashariki ya kati) au inaweza kuwa ni sababu ya mitazamo…
 
Hawa wafuatao ni baadhi ya double agents nguli kuwahi kutokea na balaa

*Human Khalid Al-Balawi*

Huyu jamaa alikuwa daktari kitaaluma na alikuwa raia wa Jordan, alikamatwa na mamlaka za Jordan kipindi akiwa mwanafunzi kwenye chuo kikuu cha Isntanbul nchini Uturuki baada ya kuonekana akiwa na muelekeo wa misimamamo mikali, inasemekana baadae CIA waliingilia na kumshawishi awe double agent kwa ahadi ya kusamehewa. Jamaa alikubali na CIA wakamuandaa kikamilifu kwa kazi hiyo ambapo baada ya kuiva wakampeleka Pakistan na Afghanistan na kumpa jukumuu la kufuatilia nyendo na shughuli za alqaida nchini humo.

Human aliifanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa mno na akafanikiwa kuwashawishi CIA ambao walionekana kumwamini 100%. Kumbe hawakujua kuwa aliqaida walikuwa tayari wamembadilisha na alikuwa akifanya nao kazi.

Siku moja akawaeleza kuwa alikuwa na taarifa muhimu kuhusu kiongozi wa juu wa alqaida bwana Ayman- Al-Zawahili na akawapa masharti kuwa angependa taarifa hizo azifikishe kwa viongozi wakuu wa CIA katika eneo hilo, kwakuwa walikuwa wanamtafuta sana Zawahili hawakusita kumkubalia na kumuagiza afike kwenye Ofisi za CIA eneo la Khost Afghanistan, Khalid alifika kwa kuchelewa na kutokana na kimuhe muhe cha taarifa waliyokuwa wanakwenda kuipokea basi wakasahau hadi kumkagua, kumbe jamaa alikuwa amevaa mabomu, baada ya kufika ndani kwa wakubwa jamaa alijilipua na kuua maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa CIA katika eneo hilo.
 
Ila Hitler wanamzushia tu na kukuzwa na media..sijui sababu aligusa watu wa taifa that is proclaimed as WATEULE?
Hivi kuna mtu kaua watu wengi kama Genghis Khan.?
Swala siyo kuua. Swala ni nani unayemuua...

Wajerumani mpaka leo wanalipa kwa waliyowatendea Waisiraeli. Jaribu kusema na sisi weusi tulipwe kwa dhuluma ya utumwa; dhuluma iliyoendelea kwa miaka 500+ kule bahari ya Atlantic. Huku bahari ya Hindi nako sijui miaka mingapi. Ukigusia hili suala utatukanwa na kuchekwa sana !!!
 
Juan Pujol Garsia*

Garsia alikuwa mhisipania ambaye maisha yake yalionekana kutokua na muelekeo kwani kwenye umri wa miaka 32 alikuwa ameshindwa karibia kila kitu, shule, biashara na hata familia, vyote alikuwa amejaribu na vikamshinda.

Baadae wakati wa vita kuu ya pili ya dunia aliamua kwenda kuomba kazi kwenye idara za usalama za England na Marekani lakini aligonga mwamba kwa madai mtu ambaye hakuwa na uwezo hata wa kufuga kuku angeweje kufanya kazi nyeti kama hii tena katika wakati tete. Baada ya kukataliwa akaona isiwe taabu akaenda zake kwa Wajerumani na kujifanya mmoja wa wanazi kindakindaki wa Hitler, manazi baadae walimuamini na kumpa kazi ambapo walimpangia kwenda England! Alielekea huko akipitia Porto Ureno na alianza kazi kwa kukusanya habari kwenye magazeti na redio, baadae alianza kupiga hatua kwa kusajili watu mhimu kutoka wazara ya habari na mawasiliano pamoja na masekretari kwenye wizara mbalimbali, baadae pia alifanikiwa kuingia hadi jeshini na jusajili watu huko.
 
Garsia alikuja kuumbuliwa na double agent wa kijerumani ambaye aliwatonya England juu ya uwepo wake nchini humo.

Baada ya kubumbuluka Garsia akijipeleka mwenyewe kwa M15 ambapo walikubali kuendelea kutumia mara hii wakimtumia kuwalisha habari za uongo.

Garsia anakumbukwa sana kutokana na kazi tukufu aliyoifanya wakati majeshi ya muungano wa England, Canada, Marekani na baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa yalipoanza oparesheni ya kukomboa maeneo yaliyokuwa yamekamatwa na Ujerumani na hasa katika uvamizi wa eneo la Normandy, baada ya wanajeshi wa muungano kuelekea katika eneo hilo wajerumani walipata intelejensia na wakawa wametuma vikosi kwenda kupambana na majeshi ya muungano huku vikosi vingine vikiwekwa tayari nchini ubelgiji, lakini Garsia kwa ujasiri wa hali ya juu akamtumia telegraphy na kumwambia hakukuwa na mashambulizi yoyote katika eneo hilo na kwamba habari alizokuwa amepewa Hitler ulikuwa ni uongo, kwakuwa Hitler alikuwa anamuamini sana basi akaiamini taarifa hii na akaviamrisha vikosi vyake vilivyokuwa njiani kurejea na vile vilivyokuwa ubelgiji kuendelea kubaki.
 
Da'Vinci mods huwa hawakuchoki?kubadili ID
Hata mimi hua sijui kusema ukweli.. nishawaambia waniwekee option niwe nabadiri mwenyewe [emoji3][emoji3]
Umeanza kurudia majina bila shaka umefika mwisho wa reli sasa. Hili la mwisho sijui Gratuity Tuci hata wiki halikumaliza [emoji16][emoji16][emoji16]

Nami nataka nibadili aisee. Hii Shimba hii imenichosha [emoji51][emoji51][emoji51]
 
Wengi wanachukulia hatua hii kama mwanzo wa majeshi ya muungano kuanza kujizatiti kwani hadi hapo Ujerumani ilikuwa tayari imekamata karibu ulaya nzima na ndio maana Garsia anachukuliwa kama double agent aliyefanya kazi ya kutukuka, lakini pia anatajwa kama double agent aliyetunukiwa tunzo nyingi mno kutoka pande zote yaani Ujerumani na England, baada ya vita Garsia alikwenda zake Amerika kusini ambapo alifungua maktaba na kumalizia maisha yake huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…