Rais huyo wa chama cha Republican anapingwa na mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden, ambaye alikuwa makamu wa rais wakati wa utawala wa Barrack Obama , lakini amekuwa katika siasa za Marekani tangu 1970.
Mwaka 2016 kwa mfano Bi Hillary Clinton aliongoza katika kura za maoni na kuibuka mshindi kwa kura milioni tatu zaidi ya mpinzani wake Donald Trump , lakini uchaguzi ulipofanyika akashindwa kwasababu raia wengi wa Marekani hupiga kura kwa kutumia njia ya posta hivyo basi ushindi wa kura nyingi hauwezi kukusaidia kushinda uchaguzi.
Amekuwa akijipatia asilimia 50 katika wiki za hivi karibuni na amekuwa akiongozi kwa pointi 10 mara kadhaa lakini bwana Trump amejitahidi na kuweza kuongeza umaarufu wake katika siku chache zilizopita.
Tofauti ni kwamba mwaka 2016, kura hizo hazikuwa wazi kama ilivyo sasa na ni asilimia ndogo iliyowatawanya Trump na mpinzani wake wa Democrat Hillary Clinton kwa alama kadhaa wakati uchaguzi ulipokuwa ukikaribia.
Hello Bro SHIMBA YA BUYENZE natafuta kitabu cha Purple hibiscus kimeandikwa na Chimamanda Adichie Ngozi naomba unisaidie kama unacho kwenye maktaba yako
Haya ndio maeneo ambayo uchaguzi utashindiwa na kupotezwa kama majimbo yanayogombaniwa. Katika mfumo wa uchaguzi wa Electoral College, unaotumiwa na Marekani kuchagua rais wake, kila jimbo hupatiwa idadi ya kura kutokana na idadi ya watu . Takriban kura 538 za Electoral College zilizopo zinawaniwa hivyobasi kila mgombea anahitaji kushinda kura 270.
Kufikia sasa, kura za maoni katika maeneo yanayowaniwa zinamuonesha Joe Biden akiwa kifua mbele, lakini kuna muda mwingi kabla ya uchaguzi huo kufanyika na huenda mambo yakabadilika haraka , hususan wakati Donald Trump atakaposhirikishwa.
Kura hizo za maoni zinasema kwamba Bwana Biden anaongoza katika jimbo la Michigan, Pennsylvania na Wisconsin - majimbo matatu ambayo mpinzani wake wa Republican alishinda kwa tofauti chini ya asilimia 1 ili kupata ushindi 2016.
Masoko ya kamari ,hatahivyo hayajamfutilia mbali rais Trump . Katika Fursa tatu za hivi karibuni masoko hayo yanampatia rais Trump ushindi wa fursa moja mnamo mwezi Novemba.
Mkosi wa rais Trump unawafanya wapinzani wake kuwa thabiti.
Mlipuko wa virusi vya corona umetawala vichwa vya habari nchini Marekani tangu kuanza kwa mwaka huu na hatua zilizochukuliwa na rais huyo zimegawanya hisia kulingana na vyama.
Wanaounga mkono siasa yake waliongezeka katikati ya mwezi Machi baada ya kutangaza hali ya tahadhari na kutoa dola bilioni 50 katika majimbo kuzuia kusambaa kwa maradhi hayo.
Wakati huo, asilimia 55 ya Wamarekani waliunga mkono hatua yake , kulingana na data za Ipsos, kampuni kubwa ya kura ya maoni duniani.
lakini uungwaji mkono wowote alioupata kutoka kwa Democrats ulipotea baada ya hatua hiyo huku wafuasi wa Republican wakiendelea kumuunga mkono rais wao.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.