Huo ndio uliokuwa uwezo wa Shakuntala Devi kufanya hesabu kwa kutumia ubongo wake kwa sekunde kadhaa hali iliowafanya wale waliomfahamu kumuita 'Kompyuta'.
Talanta yake na nambari ilimsaidia kujipatia nafasi katika rekodi za dunia za Guiness na kumfanya kuwa mtu maarufu aliesafiri kote duniani akionesha uwezo wake wa kutatua hesabu katika vyuo vikuu, kumbi za filamu, katika radio na katika studio za runinga.
Maisha ya mwanamke huyu wa India , aliefariki 2013 akiwa na umri wa miaka 83, yalioneshwa katika filamu ilio na jina lake ambayo ilitolewa hivi karibuni katika ukumbi wa Amazon.
Hakuwa na elimu, lakini alikuwa na kipaji cha kutatua hesabu ngumu zaidi kwa kutumia ubongo wake kwa kasi ya kushangaza. Alikuwa na kasi kama ya kompyuta'' ,Balan aliambia BBC.
Ili kuandaa jukumu lake , muigizaji huyo alijifunza miongoni mwa masuala mengine kanda ya video kutoka kwa runinga ya Canada ambapo Devi anaonekana akiliuliza jopo iwapo linataka kupatiwa majibu kuanzia kushoto hadi kulia , au kutoka kulia hadi kushoto.
Sekunde chache kabla, mmoja ya wanajopo hilo alikuwa amemuuliza kuzidisha nambari mbili za nambari nane. Devi aliwapatia jibu mara moja.Kanda hiyo ya video imesambazwa zaidi ya mara nusu milioni tangu ilipochapishwa mwaka 2013.
Babake ambaye alikuwa mchezaji wa sarakasi, aligundua kipawa hicho wakati walipokuwa wakicheza karata na kubaini kwamba msichana huyo mdogo alikuwa akimshinda kwasababu alikuwa na uwezo wa kukariri karata zake.
Akiwa na umri wa miaka 6 , ambapo alikuwa ametambulika kama mtoto aliependa hesabu, alionyesha ujuzi wake kwa mara ya kwanza katika hafla ya umma katika mji wa Mysore, Karnataka, Mji wa India alikozaliwa.