7. Watu
Rasimali ya mwisho ambayo tutaijadili siku ya leo, ni kuhusu watu ambao wanakuzunguka. Kila kitu huwezi kufanya kitu bila kushirikisha watu. Kama ni biashara inahitaji wateja, kama ni shule inahitaji wanafunzi, kama ni kanisa au mskiti nalo linahitaji watu pia. Hivyo ni vyema ukaweza kuwatumia watu mbalimbali kuweza kufikia lengo lako. Kama unataka mfanyabishara tunachotegemea kuona kwako ni kuona rafiki zako wakubwa ni wafanyabishara wenzako.