Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Da'Vinci

Faviola alikuwa na umri wa miaka miwili wakati anafariki Sept 6, 2018, mama yake Saundra Gonzales akaanza kuwa na wasiwasi na watu baada ya baadhi ya vitu katika kaburi la mtoto wake kama maua na midoli kuibiwa katika makaburi ya the Masonic huko Las Cruces, New Mexico alikozikwa.

Hofu hiyo ilipelekea Saundra kufunga kamera kwa siri kurekodi kama kuna matukio yoyote hufanyika katika kaburi la marehemu mwanaye usiku.

Kilichoonekana kunaswa katika kamera hiyo ni picha na video ya msichana mdogo akiwa anatembea tembea kando ya kaburi hilo, baada ya Saundra kuitazama picha hiyo akaanza kulia akidai kuwa binti huyo anayeonekana ndiye binti yake aliyezikwa.

Katika video nyingine ilionyesha msichana huyo mdogo akitembea na mwanaume mrefu katika viunga vya makaburi hayo.

"Nadhani alikuja kumchukua mwanangu ampeleke mbinguni," alisema Saundra. Hakuna uchunguzi uliofanikiwa na kutoa majibu kuhusu tukio hilo la ajabu.

Kifo cha mtoto huyo kilisababishwa na kipigo alichopewa na baba yake wa kambo Lalo Anthony aliyekuwa ni mpenzi wa mama yake, licha ya kukimbizwa hospitali lakini hakupona.
 
Urefu wa Ukuta wa China "The Great Wall" ni km 21,196 (Umbali sawa utoke Dar kwenda Mwanza, Kisha urudi tena Dar kwa kutumia gari na ufanye hivyo kwa kurudia safari mara 19), Mpaka unakamilika ulitumia takribani miaka 2,000.
 
Hard drives' za kisasa zinahitaji utunzaji wa umakini zaidi kutokana na namna zilivyotengenezwa, inaweza kupunguza ufanisi wake kikazi kwa kuipigia makelele/Kuifokea au hata kuipigia tarumbeta kwa karibu unaweza kuiharibu moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom