Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ligi Kuu ya England 2020/21 unatarajia kuanza Jumamosi ya Septemba 12, 2020. Kampeni za msimu huo wa 29 awali ulitakiwa kuanza Agosti 8, lakini kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, umebadili kalenda ya soka na sasa msimu huo mpya utaanza wiki sita baada ya kumalizika ule uliopita wa 2019/2020.
 
ZILIZOPANDA NA KUSHUKA
Leeds wamerejea katika Ligi Kuu baada ya kutokuwepo kwa takribani miaka 16, wakati West Brom ilipata nafasi ya pili ya kupanda moja kwa moja baada ya kupata nafasi hiyo siku ya mwisho ya fainali ya Ligi Daraja la Kwanza.
 
Msimu mpya wa Ligi Kuu uliahirishwa awali kutokana na kuenea kwa maambukizi ya corona nchini kote lakini Waziri Mkuu Boris Johnson ana matumaini itatoa nafasi kwa mashabiki kurejea viwanjani katika matukui ya michezo nchini England kuanzia Oktoba 1.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…