Hivyo ni wakati wako sasa wa kuipa nguvu ya kushukuru nafasi ili ivute na vile usivyokuwa navyo au ifanye nguvu hii ya kushukuru kuwa chuma ulete wa mambo mengine na vitu vingine katika maisha yako leo.
Nidhamu binafsi ni Utaratibu au sheria anayojiwekea mtu katika kufanya au kutofanya kitu au jambo fulani katika maisha yake na kutimiza Malengo yake na kutatua changamoto mbalimbali kwa jamii yake....
.Hiyo nidhamu binafsi ndio Dira ya kila kitu maana nidhamu huchora mstari ambao utaonesha wapi upite na wapi usipite katika safari ya kufikia mafanikio yako .
1.Nidhamu Binafsi humfanya mtu kujitathimini wapi Ametoka,wapi Alipo na wapi Anahitaji kufika na Wajibu wake nini katika maisha yake na jamii kwa ujumla
2.Nidhamu Binafsi itamfanya mtu kutimiza malengo yake aliyojiwekea maana kuna mstari aliyojiwekea ambao unaonesha mambo gani afanye na mambo gani asiyafanye ili kufikia kile anakihitaji juu yake.
3.Nidhamu Binafsi itamfanya mtu kujiamini kwasababu anapenda kile anachokifanya hana hofu na ana uhakika na kile kitu anachokifanya hivyo mtu huyo kufanikiwa kwake ni haraka sana .
Tena ulikuwa na mtaji mdogo sana lakini ulijituma na kupata mafanikio kwa haraka sana lakini leo umepoteza ramani yako kwa kukosa Nidhamu Binafsi na kuona kama vile unarogwa au huna bahati .
Ndugu yangu ni wakati wako sasa wa kuamka na kujikumbusha mbona zamani nilifanikiwa sana katika eneo fulani ,kwanini leo hii nafeli na wakati mimi ni yuleyule niliyefanya kipindi kile?