Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Reposted from @millardayo Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kiranyi Arusha Veronica Kidemi amesema Mume wake amemkata kiganja chake na kukitenganisha kabisa na mkono kutokana na wivu wa mapenzi. “Mume wangu amekua akinituhumu mara nyingi kwamba anasikia nina chepuka kwenye mapenzi lakini nilishamwambia anipe ushahidi na sio tu kusema anasikia na sio kila Mtu anapenda ndoa yake kuwa na amani, Yeye anafanya kazi Dar... juzi aliniambia nikachukue kilichochangu nifungashe” “Juzi Ijumaa niliporudi nyumbani akawa amerudi bila taarifa, akanikimbilia na kuanza kunishambulia niliishiwa mpaka pozi, alinikatakata kama anafyeka, alikua hataki hata niende kwa Ndugu yangu, hata nikiongea na Baba yangu anakasirika anasema mna ajenda gani ya siri mmeongea muda mrefu hivyo?” “Mpaka Mama yake anamwaambiaga aache huo wivu, mpaka Watu kazini wananikimbia wanaogopa kunisalimia sababu yake, ni wivu yani hata ukienda dukani anakuuliza kila saa uko wapi, akiniuliza kama nipo nyumbani atataka aongee na Watoto kuthibitisha” Veronica anasema amekaa na Mume huyo kwa miaka sita na wamefanikiwa kupata Watoto wawili.. “Amekua ni Mtu wa kusafiri aliwahi hata kwenda Dubai akakaa mwaka, anasafiri sana hivyo ni Mtu wa kusikiliza sana ya kuambiwa” Kamanda wa Polisi Arusha Salum Hamduni amethibitisha kutokea kwa tukio hili na kusema tayari wamemkamata Mtuhumiwa baada ya kutorokea Dar es salaam, video nzima ya Veronica akisimulia ipo kwenye youtube ya ‘millardayo’ #
 
FB_IMG_1583724968531.jpg
 
Back
Top Bottom