Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Inaaminika ni matokeo yaliyotokana na majeraha ya kawaida ya misuli na mifupa, ikiwamo kazi tunazozifanya katika maeneo yetu ya kazi na mienendo na mitindo ya kimaisha ikiwamo kutofanya mazoezi ya mwili.
 
Vilevile uzito uliokithiri, uvutaji tumbaku, kuongezeka uzito kipindi cha ujauzito, shinikizo la kimwili, kutofanya kazi, mkao wa ovyo na ulalaji usioendana. Haya ni miongoni mwa mambo yanaambatana na maumivu ya mara kwa mara ya mgongo.
 
Mengine ni santuri za mgongo kujipenyeza katika uti wa mgongo, kuvunjika kwa vifupa vya mgongo, mfano kumomonyoka kwa vifupa. Yapo mambo mengine yanayosabisha ingawa ni nadra sana ni saratani au uvimbe au uambukizi ikiwamo TB ya mgongo.
 
Karibu nusu ya wanawake waliowahi kuwa wajawazito hupata tatizo la maumivu ya chini ya kiuno wakati wa ujauzito. Hii ni kutokana na mabadiliko ya ujauzito yanayosababisha kuwa na mkao usio wa kawaida na mgandamizo wa misuli na nyuzi zinazoshika mifupa ya kiuno na mgongo.
 
Ajali zilizoambatana na umri mkubwa au matumizi ya muda mrefu ya dawa jamii ya corticosteroidi huashiria kuvunjika kwa pingili za mifupa ya mgongo. Kuwa na maumivu makali sana ya chini ya mgongo kwa mtu aliyewahi kufanyiwa upasuaji mwaka uliopita.
 
Uwapo wa homa kali, uambukizi njia ya mkojo, upungufu wa kinga mwilini, utumiaji wa dawa kwa njia ya mshipa, ni viashiria vya uwepo wa maumbukizi mwilini. Mambo haya ni viashiria hatari kuwa mwilini kuna tatizo kubwa hivyo hatua za haraka zinahitajika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…