Zifuatazo ni athari za kuvaa viatu vyenye visigino virefu wakati wa ujauzito:
Maumivu ya misuli ya mapaja.
Wadada hupenda kuvaa “high heels” husababisha misuli ya mapaja kukaza na kuwa na muonekano mzuri. Katika ujauzito, mabadiliko ya homoni huweza kupelekea misuli hii kuwa na maumivu tofauti na ilivyokua kabla ya ujauzito.
Maumivu ya mgongo.
Wakati wa ujauzito, uzito mkubwa huhamia mbele na misuli ya nyonga hulegea. Mabadiliko haya ya kimsawazo huweza kusababisha maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo na kiuno.
Hatari ya kuanguka.
Ni wazi kuwa uzito huongezeka wakati wa ujauzito na mabadiliko ya vichocheo vya mwili huweza kupelekea kizunguzungu cha hapa na pale. Hii huongeza hatari ya kuanguka iwapo utavaa “high heels” na kupelekea majeraha kwako na kwa mtoto aliyeko tumboni.
Uvimbe miguuni.
Ni jambo la kawaida miguu kuvimba wakati wa ujauzito. Kuvaa viatu vyenye visigino virefu na vyenye kubana huweza kuongeza tatizo hilo na kupelekea maumivu.
Mimba kutoka.
Mjamzito akivaa viatu vyenye visigino virefu anakua katika hatari kubwa ya kuanguka. Hii huweza kusababisha majeraha makubwa kwa mtoto aliyeko tumboni hali inayoweza kusababisha mimba kutoka.
Lakini, iwapo kuna ulazima sana wa kuvaa viatu hivyo, unapaswa kuzingatia yafuatayo:
Ni salama kuvaa viatu hivi katika muhula wa kwanza wa ujauzito (Miezi mitatu ya mwanzo).
Rosela ni ni maua yanayo julikana kabisa pia huoeshwa au kupandwa mazingira ya kawaida haswa nyumbani, maua haya yanapatikana kirahisi katika nyumba za ndugu, jamaa na marafiki na sehemu zinginezo japo kuwa baadhi ya watu huyaita maua damu.
Dawa ya magonjwa mbalimbali kama kushusha presha, sukari, uric acid mwilini, inatibu kikohozi na mafua, ina punguza mwili pia hutengeneza ngozi na kuifanya iwe laini.