Mdada, Mkaka, Mmama, Mbaba n.k.
Haya ni maneno yaliyozoeleka katika jamii yetu hivi leo. Maneno haya
yametokana na uambishaji usio sahihi wa maneno. Watu wengi bila kujua
wamejikuta wakitumia maneno haya kama maneno yasiyokuwa na dosari yoyote.
Ukweli ni kuwa maneno haya siyo sahihi.
Mfano:
Mdada aliyekuja jana ni ndugu yangu.
Huyu mkaka anafanya kazi benki kuu.
Mmama na Mbaba mmoja tu, ndio waliohudhuria kwenye mkutano.
Sentensi sahihi zingekuwa:
Dada aliyekuja jana ni ndugu yangu.
Huyu kaka anafanya kazi benki kuu.
Mama na baba mmoja tu, ndio waliohudhuria kwenye mkutano.