Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwisho wa siku

Kuna maneno mengine ambayo yamechukuliwa tu kutoka kwenye lugha nyingine na
kuingizwa kwenye lugha ya Kiswahili. Maneno “mwisho wa siku” siyo maneno
sanifu kwani yamechukuliwa moja kwa moja toka kwenye maneno ya Kiingereza
“At the end of the day”.

Mfano:

Mwisho wa siku utapata faida kutokana na kazi yako.

Sahihi ni:

Hatimaye utapata faida kutokana na kazi yako.
 
Mashule na Mahosipitali

Mara nyingi maneno haya pamoja na mengine yanayofanana nayo yametumiwa
katika miktadha mbalimbali bila kubainika kuwa siyo sahihi.

Maneno haya yanatokana na kutengeneza maumbo ya umoja na wingi katika
maneno yasiyokuwa na sifa hiyo.

Mfano:

Mashule yote yamejengwa kwa misaada ya wafadhili.

Mahosipitalini hakuna dawa za kutosha.

Sentensi sahihi:

Shule zote zimejengwa kwa misaada ya wafadhili.

Hosipitalini hakuna dawa za kutosha.
 
Utamaduni

Utamaduni ni neno lingine ambalo ni sanifu katika lugha lakini mara
nyingine hutumiwa vibaya. Maana halisi ya utamaduni ni mwenendo wa maisha
unaohusisha asili, mila, desturi, jadi au itikadi inayotawala katika jamii
fulani. Hivyo siyo sahihi kutumia sentesi kama hii.

Mfano:

Wasanii hawa wataimba nyimbo za utamaduni.

Sentensi sahihi ni:

Wasanii hawa wataimba nyimbo za asili.
 
Tetesi

Maana halisi ya neno tetesi ni taarifa ambazo bado hazijadhibitishwa.
Lakini watu hulitumia neno hili kinyume na maana halisi.

Mfano:

Ufisadi uliofanyika kwenye sekta ya madini uliibua tetesi nyingi za
malalamiko kutoka kwa wahisani.

Sentensi sahihi:

Ufisadi uliofanyika kwenye sekta ya madini uliibua malalamiko mengi
kutoka kwa wahisani.
 
Bawaba na bawabu

Bawabu na bawaba yote ni maneno sanifu ya Kiswahili lakini mara nyingine
hutumiwa vibaya.

Mfano:

Bawabu za mlango huu zimeharibika.

Nimekwazika kwa sababu bawaba alichelewa kufungua mlango.

Bawaba ni kifaa kiwekwacho kwenye mlango, sanduku au dirisha ili
kuliwezesha kufunguka na kufungwa. Wakati neno bawabu ni mtu au mlinzi
anayekaa mlangoni ili kufungua na kufunga mlango au lango. Hivyo sentensi
sahihi ni:

Bawaba za mlango huu zimeharibika.

Nimekwazika kwa sababu bawabu alichelewa kufungua mlango.
 
Dhumuni, Pito, Fao

Haya ni maneno yaliyotokana na maneno yasiyokuwa na maumbo ya umoja; hivyo
huwa si maneno sanifu pale yanapowekwa katika maumbo ya umoja.

Mfano:

Dhumuni la barua hii ni kukujulia hali.

Nina pito gumu sana maishani mwangu.

Tutakupa fao lako la uzeeni kwa wakati.

Sentensi sahihi:

Madhumuni ya barua hii ni kukujulia hali.

Nina mapito magumu sana maishani mwangu.

Tutakupa mafao yako ya uzeeni kwa wakati.
 
Usajilii na udahili

Maneno haya yamekuwa yakitumiwa sana na watu wa ngazi za elimu ya juu
pamoja na taasisi zake. Mara nyingi huchanganywa kimatumizi, hivyo
kusabaisha mkanganyiko kwa wasomaji au wasikilizaji. Ni dhahiri kuwa,
maneno haya yana mana tofauti. Udahili ni mchakato wa kumruhusu mtu
kujiunga na chuo au taasisi bada ya kuridhika na sifa zake. Usajili ni
kitendo cha kuingiza kitu au mtu katika orodha maalumu. Hivyo usajili huwa
ndiyo hatua ya mwisho katika mchakato wa kuwapokea wanafunzi chuoni.
 
Sawasawa
 
Ukiwa kama mzungumzaji au mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili
unaetaka kuwa mahiri katika lugha ni lazima uyaepuke makosa haya. Pia
vyombo vya habari ni lazima viwe mstari wa mbele kujenga lunga na siyo
kubomoa.
Kiswahili kilinifanya nis(i)ijue kabisa kuongea (lugha) (ya) Kiingereza.

Maneno ya kwenye mabano yakiwepo yanaleta maana nzuri ya sentensi. Lakini huwa mara nyingi tunatumia maneno machache sana katika maongezi yetu ya kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…