Ronald Wayne moja ya mwanzilishi wa kampuni ya Apple aliuza hisa zake kwa takribani Tsh 1,855,008.48 mwaka 1976, Ambapo kama angebaki na hisa zake hizo kwa sasa zingekuwa na thamani ya takribani Tsh 81,165,767,946,420.50
"Tendo la ndoa" humfanya mwanamke kuonekana mrembo zaidi, Kiwango cha Estrogen huongezeka ambapo hupelekea nywele pamoja na ngozi kuwa nyororo maradufu.
Watu wanaotumia mkono wa kushoto huwa na uwezo mkubwa zaidi kimaamuzi kuliko wanaotumia mkono wa kulia hasa kwenye michezo kama magemu ya video, mpira, tenisi n.k
Baadhi ya watu maarufu duniani ambao walikuwa wanatumia mkono wa kushoto, Napoleon, Da Vinci, Michalengelo, Einstein, Newton, Bill Gates, Oprah Winfrey, Obama..Ongeza wengine unaowafahamu!
Miaka ya nyuma kabla ya maendeleo ya mitandao ujio wa Filamu zinazotazamiwa kuachiwa hapo baadae zilikuwa zinaoneshwa mwanzo na mwishoni mwa Filamu nyingine ambayo unatazama (Unataka kutazama), Ndipo jina Trailer' lilipoanza kutumika kumaanisha hivyo.
Joe Biden anakuwa Rais wa kwanza kuingia madarakani akiwa na umri mkubwa zaidi (Miaka 78), Pia Kamala Harris anakuwa mwanamke wa kwanza kuwa Makamu wa Rais wa taifa hilo.