Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Klabu ya Simba imemtambulisha beki Peter Muduhwa raia Zimbabwe.Muduhwa ambaye alikuwa anachezea Highlanders F.C ya Zimbabwe amejiunga na kikosi hicho akitokea Cameroon kwenye kikosi cha Zimbabwe ambacho kinashiriki CHAN.
 
Nguli wa muziki Afrika Koffi Olomide maarufu Mopao, ametua Bongo usiku wa kuamkia leo, kwaajili ya kukamilisha collabo yake na African Princess Nandy.
Baada ya kumpokea mgeni wake, Nandy amedokeza jina la ngoma hiyo kuwa ni 'Leo leo' na ameweka wazi kuwa yeye na timu yake wamefanya uwekezaji mkubwa sana kwenye project hiyo, hivyo mashabiki watarajie kitu kikubwa.
 
John Tarimo, mkazi wa Kijenge Mwanama mkoani Arusha yupo chini ya ulinzi wa polisi kwa madai ya kutaka kujiua. Tarimo ambaye amelazwa Hospitali ya Mount Meru amejikata uume na kutaka kujiua kwa wivu wa mapenzi. Inadaiwa kumekuwa na ugomvi kati yake, mkewe na ndugu zake (Tarimo).
 
Mara nyingi tumezoea kuona maadui wengi wa MAFANIKIO yetu ni wale watu tunao waona kwa nje na wanapelekea wewe kutosonga mbele au wanaleta kikwazo juu ya kufanikiwa kwako hivyo kufanya usikae nao karibu.
 
1.Malengo yasiyo eleweka .
Katika vita wanao shinda ni wale wenye lengo vita linaloeleweka ndio wanaoshinda vita,huwezi kumpiga adui kama hujui unampigaje,hata kwenye vita ya kufanikiwa pia kunahitaji malengo yanayoeleweka na yaliyo thibitishwa ili iwe rahisi kuyafikia na kuibuka kidedea .Hivyo 2021 ni wakati wa kumpiga adui malengo ya siyo eleweka
na kuamua kufanya malengo yaliyoandikwa na yenye ukomo wa muda.
 
2.Kukosa nidhamu.
Adui huyu amekuwa akiwashambulia wengi katika nyanja mbalimbali za kifedha,kiuongozi,kibiashara, n.k ukweli ni kwamba hata uwe na malengo makubwa na mazuri ,uwe na hamasa kubwa kiasi gani kama huna nidhamu sahau kufikia kilele cha mafanikio yako ,ili uweze kutoka na kumpiga adui wa mafanikio yako unahitaji kuwa na nidhamu katika kile unategemea kuwa.
 
3.Bora Rafiki
Siyo kila Rafiki anafaa kukufanya wewe ufikie mafanikio yako.kuna marafiki ni sumu, kazi yao ni kuua ndoto yako ili tuu mfanane kimaisha, Hivi hujawahi shuhudi mtu alikuwa na maisha yake mazuri lakini alipojiunga na jamaa yake akafirisika nakutoka kwenye ramani ya kufanikiwa.
Rafiki bora ndio chaguo la wewe kuvuka na kufikia kile unahitaji kuwa
Mwaka 2021 ni wakati wa kukata mtandao wa Bora Rafiki na kuunda mtandao wa kukufikisha kule umekusudia nao ni mtandao Rafiki Bora.
 
4.Kukosa Hamasa
Adui huyu anakaa ndani ya mtu ambako chemichemi za mawazo,malengo ,maarifa ,akili, hutokea.
Ukikosa hamasa ni sawa na mua usiyokuwa na sukari japo utaitwa mua lakini hautakuwa na tija kwa mlaji maana hauna sukari.
Hivyo unahitaji kumsha hamasa yako juu ya ndoto yako ili uweze fanikiwa.
 
5.Imani potofu
Adui huyu kazi yake ni kuua uwezo wa mtu katika utendaji wake na kushindwa kufikiri vizuri maana ana amini waliofanikiwa ni wachawi au wanatumia ndumba hivyo akisha kuamini anategemea nduma ndizo zifanye kazi yake .Neno la Mungu linasema asiyefanya kazi na asile je wewe ni mtu gani ambaye utafanikiwa bila kufanya kazi.
 
6.Uvivu na uzembe
Adui huyu amekuwa akiwapiga sana wale ambao bado wanahitaji kufikia kilele cha mafanikio yako,yaani unaweza shangaa tajiri anawahi kazini na kufanya kazi kwa bidii japo anafedha nyingi na miradi mingi lakini masikini ana amka anavyotaka ,kazi afanyi kwa ubora na ndio maana adui huyu hujichukulia point tatu muhimu ,
Mtu anapoteza fedha eti anajipa moyo kuwa ni muda sijatoa sadaka hivyo pesa aliyopoteza ametoa sadaka badala ya kukiri kwamba si mtunzaji na hayuko makini juu ya fedha zake.Sadaka haitolewi kwa.mtindo huo ndugu yangu.
Acha uzembe
 
Back
Top Bottom