Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hata hivyo wewe bado unapozungumzia mlango akili yako moja kwa moja huangalia tuu Hicho ambacho sote huwa tunasema mlango ila kiukweli MLANGO ni jumla ya vyote vinavyofanya nyumba au chumba chako kijihifadhi kwa kuzuia kuingia kwa urahisi.
 
Ndio maana kama ukiishi eneo tofauti, ukawa na marafiki tofauti, ukapata elimu tofauti , ukawa na mpenzi/mke/mume tofauti, pengine wewe wa leo sio yule utakayekuwa wa wakati ujao.
 
Kwanza kabisa, je na wewe ni mmoja wa watu "wanaotafuta" maisha ? Ni kawaida kuwasikia watu wakisema wanatafuta maisha. Hii ni dhana inayopotosha kufanya watu wengi waamini kuwa maisha ni kama kitu fulani kinachowezekana kufikiwa, yaani maisha ni dhana tofauti na wewe.
 
Kuta ulizojiwekea katika maisha
Pili unatakiwa uondoe "kuta" ulizojiwekea wewe mwenyewe katika kupiga hatua zaidi za kimaisha. Soma vizuri, nimesema katika kupiga HATUA zaidi za KIMAISHA. Sio katika KUTAFUTA maisha. Kuta hizo ni kama vile uwoga wa kushindwa, Uwega wa Maumivu, Uvivu na Kujitegemeza kwa wengine.
 
Ni kweli ni mara ngapi umeweza kufanikiwa katika jambo ambalo hapo awali ulidhani usingeliweza ? Na je, ni wapi uliona mafanikio yamekuja bila kuwepo na mapungufu katika njia ya kufikia mafanikio hayo? Utajiuliza, sasa ikiwa makosa nitajaribu na kushindwa nitakuwa nimepoteza vingi sana, itakuwaje ? Swali hilo bado linadhibitisha kuwa unao uwoga.
 
Amini kuwa baada ya kushindwa, kutatokea njia mbadala au utakuwa umejifunza zaidi ili usikosee tena. Swala la kuogopa hasara linakupa shida, ila kumbuka nafasi za kushindwa ni chache pia, na hata utakaposhindwa utakuwa umejikusanyia uzoefu wa kushindana na kushindwa. Hivyo wakati mwingine hautoogopa, na pengine utaweza kupambana vema na kushindwa.
 
Uvivu ni adui yako mkubwa, hata hivyo pengine umemkaribisha na amekuwa kama sehemu ya wewe. Unachotakiwa kutambua ni kuwa ili mambo yafanyike ni lazima YAFANYIKE, hakuna cha ziada, hivyo basi FANYA, usiwe mtu wakusema NITAFANYA. Ni vema kuanza kidogo kidogo kuliko kusubiri majuto, ya kujiambia "ningejua".
 
Jambo lingine ambalo unafanya pengine kila siku ni kujishusha bila kukusudia. Mara ngapi ungeweza kujisomea ili kupata ufahamu fulani hata hivyo ukajiambia 'aah ntamuuliza fulani', mara ngapi ungeweza kujiwekea akiba ili kutimiza kusudio lako la kununua kitu fulani hata hivyo ukajisemea "aah ntamuomba fulani". Yaani hata haupati shida ya kujiuliza kama kweli hayo unayodhani wengine wafanye kwa ajili yako wewe mwenyewe unaweza kufanya. Hali hii ni pacha wa kufikia wa UVIVU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…