Winga wa England na klabu ya Leicester City , Demarai Gray, 24, ameridhia masharti binafsi na Bayer Leverkusen lakini klabu hizo mbili vinavutana kuhusu ada. (Bild -in German)
Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Sergio Ramos, 34, bado hajakubali mkataba mpya na Real Madrid, mwezi mmoja baada ya pande hizo mbili kukutana kujadiliana kuhusu kuongeza mkataba wake, ambao utakwisha msimu huu. (Marca)
Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Sergio Ramos, 34, bado hajakubali mkataba mpya na Real Madrid, mwezi mmoja baada ya pande hizo mbili kukutana kujadiliana kuhusu kuongeza mkataba wake, ambao utakwisha msimu huu. (Marca)
Mshambuliaji wa Wolves Patrick Cutrone, 23, anajiandaa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Valencia kwa msimu wote uliosalia baada ya uhamisho wake kwa mkopo katika klabu ya Fiorentina kumalizika mapema. (Mail)
Kocha wa Newcastle Steve Bruce amesema klabu itasikiliza ofa zinazoshawishi kwa ajili ya ''mchezaji yeyote'', akiwemo kiungo wa kati wa Uskoti Matt Ritchie,31, kama dau litaridhisha .( Chronicle)
Klabu hiyo ya Pep Guardiola hakina mpango na mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Bayern Munich David Alaba, 28, kwa kuwa klabu inampango wa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ushambuliaji. (Manchester Evening News)
Southampton wanajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Ansley Maitlan-Niles,23, kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili la mwezi Januari kufungwa Jumatatu. (Sun)
Manchester City wanakaribia kuwasajili makinda mawili wa Fluminense na raia wa Brazil Kayky na Metinho, wote wenye umri wa miaka 17, kwa kitita cha pauni milioni 9. (Goal)