sisi walalahoi bado tunaendelea na tafakari juu ya maisha ya almarhum, kipindi hiki yatasemwa mengi juu yake kutoka ndani ya vifua vya wanadamu
=================
BURIANI KAKA YANGU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD
SEHEMU YA KWANZA.NILIVYOKUTANA NA MAALIM SEIF
Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, 19 Februari 2021.
Nimepokea kwa masikitiko, simanzi na huzuni kubwa sana taarifa ya kifo cha Maalim Seif Shariff Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, na Mwenyekiti wa ACT-WAZALENDO; Kilichotokea Jumatano Februari 17, 2021.
Mara ya kwanza nilikutana na Maalim Seif Sharif Hamad mwezi Julai au Agosti 1973, msikitini, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.