SEHEMU YA PILI: MAALIM SEIF ANISHAURI NISIGOMBEE URAIS KWA TIKETI YA CUF
Mwaka 1993, CUF chini ya Uongozi wa Mwenyekiti James Mapalala, Makamu Maalim Seif Sharif Hamad, na Katibu mkuu Shaaban Khamis Mloo, kilifanikiwa kuwa Chama cha Upinzani cha kwanza kupata usajili wa kudumu, baada ya kukamilisha masharti ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992.
Wakati CUF inapata usajili wa kudumu mimi nilikuwa Msaidizi na Mshauri wa mambo ya Uchumi wa Rais Ali Hassan Mwinyi.
Katikati ya mwaka 1993 nilitunukiwa fursa ya kuwa Fulbright Visiting Professor of Economics, Chuo Kikuu cha Williams College, Massachussets, nchini Marekani. Niliomba rukhsa kwa Rais Mwinyi ili niweze kuitumia fursa hiyo.
Mzee Rukhsa akanikubalia, nikaenda Marekani kufundisha na kufanya utafiti kuhusu maendeleo ya uchumi.