Nitafanya makosa ikiwa ndowa nitaipa sifa ya pepo ,lakini itakuwa dhambi kubwa isiyo mfano kuinasibisha na moto,kwangu ndowa ni Safari iliyobeba maana ya safari,ndio maana waongozao Safari huwataka abiriya wao kufunga mikanda vyema kabla chombo hakijaanza kuondoka ili kukabiliana na yale yatakayojiri safarini .
Mwendo wa safari na yaliyomo ndani yake ndio hutowa matokeo ya mwelekeo wake.
Msafiri hutakiwa kuchaguwa Kwa makini chombo kitakachomfaa kumpeleka Safari yake.