Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tafiti zimebainisha kuwa mtu anashauriwa kutumia maganda ya ndimu kama ambavyo anatumia juisi ya limao kwani maganda hayo yanavirutubisho muhimu sana katika mwili wa binadamu hasa katika kupambana na kiwango cha sukari ndani ya mwili.
 
Aidha, utumiaji wa juisi ya limao kila siku asubuhi una faida kubwa sana katika mwili wa binadamu, kwani limao ina virutubisho na madini mbalimbali kama Calcium, Magnesiam, vitamin C, Zink, Potasiam, kopa, chuma na Protini.
 
Limao husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kulainisha choo, hivyo kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo la kupata haja kubwa wanashauriwa kila siku asubuhi kutumia juisi ya limao ili kusaidia kupata haja kubwa kwa urahisi.
 
Limao hutunza mfumo wa kinywa hasa kwa kujali afya ya meno, utumiaji wa limao kila siku asubuhi husaidia kubadilisha rangi ya meno yako hasa wale wenye meno ya njano ndimu husaidia kung’arisha meno nakuyafanya yawe katika hali ya kawaida ya uweupe, hivyo kwa lengo hili inashauriwa uweke vitone vichache katika mswaki wako wakati wa kupiga msawaki ili kupata matokeo hayo kwa urahisi zaidi
 
Hutunza nywele, inashauriwa wakati mwingine kuchungua kiasi fulani cha ndimu nakupaka katika nywele hii husaidia kufanya nywele zako kuwa zenye afya na kwa wale wenye nywele chache limao husaidia kujaza nywele na kuzing’arisha na kuzifanya zipate muonekano wa asilia.
 
Moja ya faida kubwa ya limao ni kupunguza uzito wa mwili, madaktari wanasisitiza kila asubuhi mtu kutumia glasi ya maji yaliyochanganywa na ndimu pamoja na asali husaidia mfumo wa kuyeyusha mafuta ndani ya mwili na kumfanya mtu apunguze uzito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…